Tuesday, August 16, 2016

Rais wa zamani wa FIFA Joao Havelange afariki dunia

Aliyekuwa Rais wa zamani wa FIFA Joao Havelange enzi za uhai wake.
Rais wa zamani wa FIFA Joao Havelange amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100. Mbrazil huyo alikuwa mtangulizi wa Sepp Blatter katika shirikisho la mpira wa miguu duniani kuanzia mwaka 1974 hadi 1998.
Alijiuzulu nafasi ya Urais wa FIFA April 2013 kufuatia uchunguzi wa madai ya kupokea rushwa, na kulazwa hospitalini mwaka uliofuata alipokumbwa na ugonjwa wa mapafu.
Alikuwa mmoja wa wanakamati wa Olympic (IOC), kuanzia mwaka 1963 hadi 2011 alipojiuzulu kwa sababu ya kudhoofu kwa afya yake.
Havelange aliiwakilisha Brazil katika mashindano ya Olympic ya Kuogelea mwaka 1936, mwaka ambao aliidhinishwa kuwa mwanasheria kabla ya kuchaguliwa na IOC.
Akiwa kiongozi wa FIFA aliongeza washiriki wa kombe la dunia kutoka timu 16 hadi 32, ambapo mashindano 6 yalifanyika chini ya utawala wake.
CHANZO: BBC SWAHILI

#MACHAS OFFICIAL SITE

No comments:

Post a Comment