Thursday, November 3, 2016

YA ULIMWENGUNI:ALIZALIWA NA MIGUU MINNE, LAKINI ANAENDESHA BODABODA! INGAWA HAFURAHII WALA KUVUTIWA NAMNA ALIVYO>>>>

Arun Kumar (22), anatokea eneo la Uttar Pradesh, nchini India ana miguu mingine ya ziada miwili ambayo imeota kwenye makalio yake ambayo inampa shida na hivyo kushindwa kutembea vizuri.Kijana huyo ambaye alizaliwa akiwa na miguu minne ameomba msaada wa madaktari ili waweze kumfanyia upasuaji na kuiondoa miguu ya ziada mwilini mwake ambapo moja kati ya miguu hiyo ni kipande kidogo na mwingine umeinamia kwenye goti lake.
Baada ya kuishi kwa muda wa miaka 15 bila kupata matibabu ya aina yeyote, kijana huyo aliamua kuomba msaada kupitia mitandao ya kijamii akitaka watu wajitolee kumsaidia ili aweze kukatwa miguu hiyo miwili ya ziada.
Alianza kupata matumaini baada ya timu ya madaktari bingwa wa mifupa kutoka Hospitali ya Fortis ya huko Delhi kukubali kumfanyia upasuaji huo.
Timu ya madaktari kwa sasa wanafanya utafiti wa jinsi ambavyo miguu yake minne imeumbwa, damu inavyotembea kutoka kwenye moyo kwenda miguuni ili waone namna ya kumfanyia upasuaji.
Arun anasema: “Kama nikifanyiwa upasuaji, na madaktari wakaondoa miguu yangu miwili ya ziada, nitaishi maisha ya furaha zaidi.
“Nitakuwa na uwezo wakutembea vizuri kama wengine.
“Nitaenda hospitali, nitakutana na madaktari. Kama watakubali na mimi nipo tayari kabisa kutibiwa.”
Mbali na kwamba miguu yake miwili ya ziada haiwezi kutembea, Arun hahisi chochote kuhusu miguu hiyo, na ana uwezo wa kubeba mizigo begani, mgongoni na kutembea kawaida hata kuendesha pikipiki.
Mama mzazi wa Arun, Kokila Devi amesema: “Wakati wa kumzaa Arun, alipatwa na maumivu makali kabla ya mtoto kupitia kwenye njia yake, lakini cha ajabu miguu yote ilikuwa inalingana lakini kadri alivyoendelea kukua miguu miwili ikawa mikubwa ya kawaida na mingine midogo.Mbali na familia ya Arun kutembea huku na huko kwa miaka mitano wakitafuta ufumbuzi wa tatizo hilo, waliamuliwa na madaktari kurudi nyumbani kujifunza namna ya kuishi na kijana huyo.
Suluali yake inamatundu matatu ya miguu.
 
prepared and edited by
 

No comments:

Post a Comment