Sunday, August 28, 2016

AFYA YA MHESHIMIWA GODBLESS LEMA IMERIPOTIWA KUWA MBAYA BAADA YA KUSUSIA CHAKULA MAHABUSU

MBUNGE WA ARUSHA MJINI,MHESHIMIWA #GODBLESS LEMA
Afya ya Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema imeripotiwa kuwa mbaya baada kususia kula chakula akiwa mahabusu tangu alipokamatwa juzi asubuhi.
Lema alikamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake juzi alfajiri na taarifa za kukamatwa kwake zilithibitishwa na Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ambaye hata hivyo hakutaja sababu za kukamatwa kwa mbunge huyo.
Imeelezwa kuwa mbunge huyo tangu akamatwe na polisi amegoma kula chakula hali iliyopelekea afya yake kuwa mbaya.

CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS LIMITED

MACHAS OFFICIAL SITE

No comments:

Post a Comment