Sunday, August 28, 2016

UHUSIANO WA CHOCOLATE NA UWEZO WA KUFIKIRI DARASANI KWA MWANAFUNZI>>>>>>>>>

CHOCOLATE
Wakati wazazi wengi nchini wakihaha kudhibiti ulaji holela wa vitu vitamu kwa watoto wao ili kuimarisha afya ya kinywa. utafiti mpya wa hivi karibuni umeibua mapya baada ya kubainika kuwa ulaji mzuri wa chocolate unaweza kuongeza uwezo wa kufikiri na hivyo kutoa fursa kwa watoto kufanya vizuri darasani.

Aidha, utafiti huo umebaini vilevile kuwa ulaji wa chocolate husaidia kupunguza kasi ya kawaida ya kuzeeka kwa walaji itokanayo na kuongezeka kwa umri. Ripoti ya utafiti huo iliyotolewa hivi karibuni, inabebwa na utambulisho usemao ‘ulaji wa chocolate huongeza utendaji kazi wa ubongo” na kwamba ”unaweza kusaidia mtu kutozeeka haraka licha ya umri kuzid kumtupa mkono’

Utafiti huo uliochapichwa mwezi huu katika jarida la Appetite, umebaini kuwa kumbukumbu na uwezo wa kufikiria ufumbuzi wa mambo magumu huwa katika kiwango cha juu kwa watu wanaokula chocolate kwa wingi. Matokeo hayo yameripotiwa kutoathiriwa na umri wa mlaji, uzito wa mwili wala aina nyingine za ulinganifu wa ujumla wa kiafya .

Inaelezwa zaidi kuwa utafiti huo unaonyesha kuwapo kwa uhusiano mkubwa kati ya ulaji wa kila mara wa chocolate na matokeo ya majaribio kuhusu uwezo wa ubongo katika kufikiri. hata hivyo utafiti huo haujathibitishwa kwa asilimia 100 juu ya uhakika wa kisayansi juu ya kile kilichobainishwa.

Aidha imeonekana watu waliotumia zaidi chocolate walikuwa na lishe bora zaidi na pia kunywa pombe kwa kiasi kidogo, na makundi yote yalitegemea uwezo wa kukumbuka mambo kupitia kiwango chao cha ulaji wa Chocolate......

 
 
#MACHAS OFFICIAL SITE
 

No comments:

Post a Comment