Monday, June 27, 2016

Nyumba 5 Kali Za Superstars

 
Kila binadamu anaruhusiwa kuota. Kupitia ndoto na kisha kuzifanyia kazi ndoto zako(hapa ndoto naweza kuzijumlisha kama vitu vyote unavyoviwaza na kuvitamani) kwa juhudi,maarifa na of course imani, kila kitu kinawezekana. Hizi hapa ni nyumba kali 5 zinazomilikiwa na baadhi ya superstars au celebrities tunaoweza kuwatambua kirahisi. Na wewe unaweza kuzimiliki siku moja. Just believe and work hard. Ipi umeipenda zaidi?
 
 
 

John Travolta anajulikana kuwa ni mpenzi wa kurusha ndege na ni pilot. Mwigizaji huyu aliyepata umaarufu kuanzia kwenye movie kama The Saturday Night Fever nk amejenga nyumba hii huko Ocala, Florida kwenda na mazingira yake na ili aweze kutua ndege zake ikiwemo Boeing 707 na Gulfstream. Aliijenga kwa dola milioni $12.5.


Nyumba ya superstar wa Barcelona na Argentina Lionel Messi. Kama unavyoiona kwa juu imetengenezwa kwa mfano wa mpira uliopo uwanjani. Ukitizama vizuri kutoka kwa juu utaona namba 10(mpira na hilo eneo kama la golini) namba ambayo anavaa superstar huyo wa Argentina. Mchoro na kila kitu kilibuniwa na Architect Luis de Garrido. Nyumba ipo Barcelona.



Price: $52 Million (2001)
Oprah Winfrey anaiita nyumba hii “Promised Land” ikiwa ni kumuenzi Dr. Martin Luther King mpigania haki za watu weusi aliyesema katika hotuba yake ya mwisho kwamba “tutaiona nchi ya ahadi”. Sehemu yote ya nyumba hii ina ukubwa wa ekari 42. Ina vyumba 6 na vyoo na mabafu 14, sehemu za kuotea moto 10, theaters 2 na vitu vingine kama ziwa la kutengenezwa, swimming pool nk




Nyumba hii ni ya mwanamuziki Celine Dion. Aliinunua kwa dola milioni $72.5 Imepewa jina la Jupiter Island mansion. Ina Water Park yake. Ipo Florida,Marekani.



Supermodel Naomi Campbell. Nyumba hii imejengwa kwa mfano wa jicho. Wenyewe wanasema ni “Eye Of Horus” kutoka Misri. Ipo katika kisiwa kidogo Uturuki. Ilibuniwa na kuchorwa na architect Luis de Garrido kutoka Hispania.

#MACHAS OFFICIAL SITE

No comments:

Post a Comment