Upande wa kuingilia abiria kwenye stendi hiyo.
Abiria wakisubiri usafiri.
BASI LIKIWA LINAINGIA...
UTARATIBU WA NAMNA YA KUINGIA STENDI HUMU UKIENDELEA
BASI LIKITOKA GETI KUU KUENDELEA NA SAFARI,BAADA YA KUSHUSHA NA KUPAKIA ABIRIA
MMOJA WA MAAGENT,AKITAFUTA ABIRIA
REPORT BY JULIE KAVISHE-JOURNALIST MACHAS BLOG:-
baada ya ukarabati wa takribani miaka miwili, hatimaye Stendi ya Mabasi ya Mikoani ya Msamvu iliyopo Morogoro imefunguliwa mwishoni mwa wiki iliyopita huku ikiwa na muonekano wa kisasa kabisa na wengine kuifananisha na uwanja wa ndege ‘Airport’
BLOG YAKO PENDWA #MACHAS_OFFICIAL_SITE imefanikiwa kutinga ndani ya stendi hiyo ya kisasa ambayo iko kwenye hatua za mwisho za kumalizia ukarabati kwa kiwango cha hali ya juu, ambapo imeweza kupiga picha zinazoonyesha namna ambavyo mandhari ya stendi hiyo inavyovutia kwa sasa tofauti na ilivyokuwa awali kabla ya ukarabati.
blog yetu imeshuhudia abiria wengi wakipanda na kushuka kwenye mabasi kama ilivyoada lakini kwa sasa wakipanda na kushuka kama wako uwanja wa ndege kutokana na mandhari ilivyo vizuri mno kiasi cha kufananishwa na viwanja vya ndege(airport), huku wengine wakiwa wanasubiri usafiri ili kuelekea sehemu mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Akizungumza na reporter wa blog hii, mmoja wa viongozi wa Stendi hiyo, ameeleza kuwa, endapo wakimkamata mtu yoyote akiwa anatupa takataka ama kukanyaga bustani atatozwa faini ya Tsh. 50,000/= papo hapo.
PHOTOS & REPORT BY
No comments:
Post a Comment