Tuesday, June 28, 2016

2016 BET Experience – BET International ‘Sounds of Africa’

VICTORIA KIMANI FROM KENYA.....

BET Award ilianzishwa mwaka 2001 na  kituo cha Black Entertainment Television, kusheherekea muziki wa African Americans na mataifa mengine (minority) katika music, filamu(Acting), michezo na sehemu nyingine nyingi katika burudani.  Award hizi  zinafanywa kila mwaka. Zinaonyeshwa Live kupitia kituo cha Television cha BET.
Shughuli ya utoaji tuzo husindikizwa na performances kutoka kwa wasanii mbalimbali. Miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza mwaka huu ni pamoja na Alicia Keys,Usher,Maxwell, Jennifer Hudson, Young Juck na wengine.
Kwa bahati mbaya hakuna msanii kutoka Afrika ambaye ata-perform kwenye main act ya tuzo za mwaka huu. Wasanii wanaopewa tuzo wakati wa tukio kubwa(main award presentation ceremony) huchaguliwa kutokana na maombi au maoni ya wengi. Mashabiki wana nguvu. Na of course hii hutegemea wadhamini pia.
Historia ya BET inasema kwamba tuzo ya kwanza kabisa kutolewa ilikuwa ni ubunifu wa mchonga vinyago Carlos Rodriguez(Mare139) Kundi/wasanii wa kwanza  kupata hiyo trophy ni kundi lililowahi kuvuma sana la Outkast. Hata hivyo mwaka 2007 Society Awards ya jijini New York ambao ndio watengenezaji wakuu wa tuzo  zinazotumika katika matukio mbalimbali, waliiboresha trophy ya BET na kuwa hii ambayo wanapewa washindi hivi sasa.
Mchanganuo wa tuzo hizi huwa namna hii; BET Academy huwapelekea watu 500 walio kwenye music industry, media, bloggers nk majina na vipengele mbalimbali vya wasanii ambao wao wanawapendekeza kuwania tuzo. Hao huwa wasanii ambao kazi zao zimefanya vizuri katika mwaka unaokuwa unaishia.
Watu hao wapatao 500(Yangaroo) huchagua majina 5  kutoka katika vipengele hivyo na kisha kuwarudishia Academy. Hapo ndipo utasikia majina ya wasanii wanaowania tuzo hutangazwa na mashabiki kuanza kushirikishwa kwa njia moja au nyingine zikiwemo za kupiga kura mitandaoni nk. Kimsingi BET Academy ndio wanaweza madaraka ya mwisho ya kuwapata washindi na runners-up nk. Kama mchango wa mpiga kura wa mtandaoni unaheshimika kwa asilimia 100% au la ni suala gumu.
Tangu mwaka 2012 BET walianzisha kitu wanachokiita BET Experience, ni matukio mbalimbali ya takribani siku 4 kuelekea kwenye tukio kuu. Kuna concerts, fashion show, dinner parties, seminars, celebrity basketball games na BET international ceremony inakuwa moja wapo ya event, kutangaza washindi wao. nk.
Mwaka huu ambao ni 2016, the 15th annual BET Experience imefanyika kuanzia (June 23-26) huko Los Angeles(L.A). Kama miaka mingine iliyopita, mwaka huu pia una shughuli kibao kama concerts pale Staple Centre, Free Fans Fest nk. Huko utakutana na watu kama Kevin hart, Nicki Minaj, Kendrick lamar, Usher na wengine wengi.Mwaka huu kutakuwa na tuzo au matukio maalum ya kuwakumbuka baadhi ya nyota waliofariki na walio hai kama Michael Jackson, Prince, Smokey Robinson, Bad Boys nk
Matukio ni mengi. Kwa upande wa Afrika bila shaka tukio ambalo linatugusa zaidi ni ;BET International “Sounds of Africa” Exhibit Grand Opening and 24th International nominee reception na BET International Ceremony. International nominee reception,  lilifanyika jana tarehe 24 Juni 2016 pale Grammy Museum Los Angeles, California. Wasanii wanaoalikwa kwenye tukio hili huwa zaidi wale ambao wameteuliwa kuwania tuzo ya BET Award International ACT wakiongozwa na Diamond Platinumz kutoka Tanzania. Wengine kwenye kipengele hicho ni Wizkid (Nigeria), AKA (South Africa), Serge Beynaud (Côte d’Ivoire); MzVee (Ghana); Cassper Nyovest (South Africa); Black Coffee (South Africa) na Yemi Alade (Nigeria)
Mbali ya performances mbali shughuli hii ilikuwa pia na fashion show ambayo iliongozwa zaidi na designer Davis Tlale kutoka Afrika Kusini. Kama kawaida Red Carpet haikukosekana.


Reality Star (USA) karlie Reed attends the BET International “Sounds of Africa” exhibit grand opening and 24th international nominee reception during the 2016 BET Experience;
 
WATCH THE VIDEO HERE:-
 
 
 
 
#MACHAS OFFICIAL SITE

No comments:

Post a Comment