Wednesday, February 3, 2016

TAARIFA JUU YA UGONJWA WA VIRUSI VYA "ZIKA"

ZIKA! UGONJWA HATARI, UNAOSAMBAA NA UTAKAOISUMBUA DUNIA?
Mtatiro J.
Trending now! Hebu Chukua muda wako ui-google hii kitu kisha urudi uijadili hapa.
...
"ZIKA" ni ugonjwa mpya na hatari sana unaokuwa maarufu siku za hivi karibuni. Kihistoria umekuwa nchini Brazil lakini sasa unahamia kwa kasi Marekani na Wataalamu wa tiba wa kimataifa wanasema muda si mrefu utaanza kuiathiri Afrika na Asia.
"ZIKA" inawafanya watoto wazaliwe na ubongo dhaifu uliotepeta na usiokua (maelfu ya watoto wameshaathirika nchini Brazili), matokeo yake ni mtoto kutokukua na kutokuwa na manufaa yoyote.
Ugonjwa huu unaambukizwa na mbu aina ya "Aedes genus" lakini kwa sasa imethibitishwa kuwa unaenezwa kwa kasi kwa njia ya "kujamiiana" na mtu mwenye virusi vya ugonjwa.
Ugonjwa huu hauna tiba, ni kama "EBOLA"! Na tayari kuna tetesi zimeenea miongoni mwa wanasayansi wakihoji huwenda virusi vya ugonjwa huu "vilitengenezewa maabara" kwa lengo maalum!
Hatutishani jamani, kazi ya mitandao ni kupashana habari na kuchukua tahadhari.
Mtatiro J.
Soma zaidi kuhusu ugonjwa huu;
http://www.reuters.com/article/us-health-zika-idUSKCN0VB145
http://www.nytimes.com/…/zika-virus-world-health-organizati…
https://www.yahoo.com/…/zika-virus-transmitted-through-sexu…
www.enockmachatz.blogspot.com

No comments:

Post a Comment