Tuesday, June 20, 2017

EBITOKE: ENDAPO BEN POL ATAKATAA,KUJIHUSISHA MAPENZINI AU KUNIOA,NITAJIUA KWA AJILI YAKE>>>>

Aliyesema mahaba niue hakukosea kabisa kwani hii imekuja kujidhihirisha kwa mchekeshaji mrembo Ebitoke ambaye karibia mwezi mmoja sasa anahangaika kuwinda penzi la Ben Pol.
Ebitoke amesema kwa sasa mahaba yake yote yapo kwa Ben Pol na endapo atashindwa kupata penzi lake basi yupo tayari kupoteza uhai wake.
“Hapana Ben Pol hawezi kuacha kuwa na mimi, nitafanya kila njia ili aweze kuwa na mimi ,”
amesema Ebitoke huku akisisitiza kuwa yupo tayari hata kujiua kwa ajili ya Ben Pol.
Hata roho nitaweza kujitoa….ndiyo nitajiua kwa ajili yake.. ndiyo nitajiua kwa ajili yake… sitofanya dhambi kwa kujiua kwa ajili yake,”amesema Ebitoke kwenye mahojiano yake na Times FM.
Hata hivyo mrembo huyo mchekeshaji haswaa amesisitiza kuwa watu wasishangae maamuzi yake ya kujiua endapo atakataliwa na Ben Pol kwani mapenzi ni upofu na yana hisia kali moyoni.

MAAJABU:KIJANA ALIPA MAHARI BAADA YA MKEWE KUFARIKI>>>>>>>>

Kijana mmoja kusini mwa Msumbiji katika mkoa wa Inhambane alilazimika kumlipia mahari mkewe aliyefariki wikiendi iliyopita. Kulingana na chombo cha habari cha taifa msumbiji, mkewe alifariki kutokana na tatizo ya kujifungua.
Ndugu wa marehemu walimshutumu kijana huyo kwa kushindwa kuafiki majukumu yake ikiwemo kutambulishwa kwa jamaa na ndugu za mwanamke huyo kabla ya kufariki.
Ili kuhakikisha kuwa mazishi hayo yaliyozuiliwa yanafanyika, kijana huyo alilazimika kumnunulia nguo na viatu mkewe aliyefariki, kukubali kulipa zaidi ya dola 800 na kufanya harusi mnamo tarehe 15 mwezi Disemba.
Ndugu mmoja wa kijana huyo Irmao do Jovem alielezea kuwa walijaribu kuchangisha fedha zilizokuwa zinahitajika na waliweza kupata dola 178 pekee, na fedha zilizobakia walihaidi kulipa siku ya harusi....

Thursday, June 15, 2017

HIZI NI PICHA ZA MASHAMBA YA MHESHIMIWA MBOWE,YALIYOHARIBIWA NA SERIKALI WILAYA YA HAI MKOANI KILIMANJARO>>>>>

 UHARIBIFU ULIOFANYWA NI PAMOJA NA,KUKATWA MABOMBA,KUCHANWACHANWA GREEN HOUSES N.K




HAYA NI MANENO ALIYOTOA MBOWE,KUFUATIA KUHARIBIWA MALI ZAKE>>>>
“Hakuna wingi wa mali ambao wataharibu utakaonifanya Mbowe nikapige magoti kama wengine wanavyopiga magoti, sitapiga magoti, nitasimama katika kweli na haki wakati wote wa maisha yangu, kwa hiyo hili halinishangazi kwa sababu najua gharama ya ninachokilipa, wako watu wengi wamenipigia simu wakijaribu kunipa pole kunitia moyo, wengine wamejaribu kunitia hofu, wakiniambia Mwenyekiti Mbowe pengine uachane na siasa, nimewaambia sitoachana na siasa, nitafanya siasa, ilimradi ni siasa safi zenye kusimamia ukweli na haki nitasimama nazo.“
 MHESHIMIWA FREEMAN HAIKAELI MBOWE
MWENYEKITI WA CHADEMA-TAIFA,MBUNGE JIMBO LA HAI KILIMANJARO,MKUU KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI.
 

Saturday, June 10, 2017

HOMA YA MAFUA YA NGURUWE(Swine Flu),YATIKISA MJI WA DODOMA NA VIUNGA VYAKE,MARUFUKU YATOLEWA>>>>>>>


HII NI TAARIFA KAMILI>>>>

NILIBAHATIKA KUSOMA SHULE MOJA NA RAIS JOSEPH KABILA WA CONGO_J'MOE(JUMA MCHOPANGA)>>>>

JAY MOE-MKALI WA HIP-HOP TANZANIA
Msanii wa Bongo Fleva, Jay Moe ameeleza changamoto alizokumbana nazo shule hadi kupelekea kutoa albamu ya Ulimwengu Ndio Mama, licha ya hiyo kuna vitu ambavyo anajivunia ikiwemo kusoma shule moja na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila.
Rapper huyo amesema kutokana na kukulia katika maisha ya kishua hadi unafika wakati ambapo anaenda boarding school alikuwa hajui kama kuna nyumba za udongo nchini zaidi ya kuziona kwenye movie za Vietnam.
Ameeleza kuwa wakati anaenda Mbeya kuanza form one mwaka 1993 ndipo alianza kuona nyumba za udongo kitu kilichomfanya kuanza kulia lakini baba yake na ndugu zake walipomueleza kuwa amekua, hivyo hana budi kuachana na mambo ya kitoto na kupambana.
“Siku ya kwanza nilipofika Irambo (secondary) jamaa waliniibia begi la mamisosi, kwa hiyo kule ndipo nilipojifunza maisha kiasi kwamba nilipofika form three mzee wangu alitaka anihamishie Dar es Salaam lakini nikamwambia hapana mimi nabaki, nimeshazoea ingawa maisha ni magumu,” Jay Moe amekiambia kipindi cha The Play List cha Times FM.
“Kingine kinacho-inspire image yangu ni kwamba, mimi nimesoma na Joseph Kabila ambaye ni Rais wa Congo, nimesoma na Cesi, nimesoma na Clara ambao wote ni watoto wa mzee Kabila.  Mimi nikiwa form two Jose ndio anamaliza form six na alikuwa kaka mkuu wa shule, kwa hiyo nilijifunza kama huna mama basi, kuna ulimwengu ambao utakufunza kama mama,” amesema Jay Moe.
H.E JOSEPH KABANGE KABILA
DE PRESEDENTE LIJUVENILE DRC
 

Thursday, May 25, 2017

BONGO FLASH:HUYU NI MSANII WA KIUME MAARUFU ANAETAMANIWA KIMAPENZI NA JAQUELINE WOLPER MASSAWE>>>>>

JACQUELINE WOLPER..
Kwenye #KikaangoniEATV Msanii wa filamu maarufu Tanzania Jacqueline Wolper amemtaja msanii wa kiume anayempenda Tanzania ila kumwambia hawezi…
Wolper amemtaja rapa mkali kutoka Arusha Joh Makini, hit maker wa ngoma kama #Waya na #PerfectCombo