Monday, February 4, 2019

BONGO VIBES: HATIMAYE OMMY DIMPOZ AMEREJEA TANZANIA KUTOKA UGHAIBUNI ALIKOKUWA AKIPATIWA MATIBABU>>>

Omari Nyembo,ommy dimpoz....MUNGU NI MWEMA SANA,KILA WAKATI TUNAMSHUKURU UMEREJEA VYEMA KUTOKA HOSPITALIN,UMEUGUA KIPINDI KIREFU MNO NDUGU YANGU,ILA ALIYETUUMBA ANATUJUA VYEMA KWA KUWA YEYE NDIYE MWENYE KUTUPA UZIMA NA PUMZI TULIYONAYO.....KARIBU SANA NYUMBANI TANZANIA,KHERI NA UPONYAJI VIZIDI KUAMBATANA NAWE......
👇👇👇
Na huu wimbo mpya uliotupa as gift and comeback to thanks God for deliverance ni mzuuuuuri mno..."NI WEWE" KWELI AHIMIDIWE YEYE MUNGU MWINGI WA REHEMA....TUKO PAMOOOOOOOOJA
By MACHAS OFFICIAL SITE.

Friday, September 15, 2017

VIDEO MPYA: RAYVANNY FROM WCB-UNAIBIWA>>>>


TRENDING IN BONGO:PICHA 14,MFAHAMU MWANAMKE ANAESADIKIWA NDIYE MPENZI MPYA WA MWANAMUZIKI DIAMOND PLATNUMZ>>>

Umesikia habari za ikulu ya Madale kufuka moshi? Sahau kuhusu Hamisa Mobetto na wengine, mshindi wa BBA mwaka 2013 (The Chase) Dillish Mathews ndio habari ya mjini kwa sasa. Mrembo huyo ambaye ni raia wa nchini Namibia anadaiwa kuuingilia utamu wa Zari The Bosslady kwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Diamond. Mfahamu zaidi malkia huyo kwa picha hizi hapa chini.
















Friday, July 7, 2017

NAY WA MITEGO,GIGGY MONEY,AMBER LULU HAWANA TOFAUTI KIMUZIKI-DUDU BAYA(MAMBA)>>>>

Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop nchini TANZANIA, Dudu Baya amedai muziki wa rapa Nay wa Mitego hautofautiani sana na muziki wa Gigy Money na Amber Lulu huku akidai ni muziki uliotawaliwa na majungu na majigambo.
Akiongea na CHANEL MOJA YA BURUDANI BONGO hivi karibuni, Dudu amewashangaa mashabiki wa muziki kuendelea kumpatia support rapa huyo wakati haoni chochote anachofanya kwenye muziki.
“Mimi sio shabiki wa muziki wa Nay wa Mitego, kwanza muziki wake haueleweki ndio maana namfananisha na Amber Lulu na Gigy Money,” alisema Dudu Baya. “Kuna wasanii wakali wanafanya muziki mzuri kuliko huyo lakini hawapewi support, mimi ningewashauri tu mashabiki wa muziki wapende muziki mzuri,”
Alisema hajui rapa huyo anafanya muziki wa namna gani kwani amekuwa ni msanii wa hip hop anayetumia mwamvuli wa hip hip kuwasema watu.
Rapa huyo amewataka mashabiki wa muziki kusikiliza muziki mzuri ambao utawajenga na sio muziki ambao ndani yake una maneno ya kuwasema watu bila sababu.

KATAZO MAALUM: NI MARUFUKU KUFUGA KUCHA NA KUJIPODOA>>>>

Kama ulikuwa una ndoto za kufanya kazi nchini Uganda hasa kwa watoto wa kike wenye kupenda kujipodoa na kuvaa nguo zinazoonyesha maumbile basi jua hautaweza kudumu wala kupata kazi nchini humo.
Hii ni kutokana na sheria mpya iliyopo, Kwa mujibu wa mtandao wa edaily wa Kenya, umeripoti kuwa serikali ya Uganda imepiga marufuku uvaaji wa nguo fupi makazini, upakaji make up uliozidi, kubandika kucha ndefu na bandia, kuweka nywele bandia na kuzipaka rangi, kuvaa nguo inayobana kama vile Tshirt na magauni pamoja na kuvaa vivalio.
Mwaka 2013 nchi hiyo ilitunga sheria ya kukataza kuvaa nguo fupi, sheria ambayo ilizua mijadala nchini humo na sehemu zingine mbalimbali lakini kwa sasa inaonekana kuanza kutekelezeka nchini humo.......

BEEF JUU YA BEEF: NAY WA MITEGO HANA CHA KUNIZIDI ZAIDI YA HELA – YOUNG KILLER MSODOKI>>>

Msanii wa hip hop Bongo, Young Killer ametoa sababu ya kusema "hana hela" katika diss track ‘True Boya’ aliyoiachia kwa ajili ya Nay wa Mitego.Rapper huyo ameeleza kuwa aliamini baada ya kumjibu Nay kupitia ngoma hiyo ni lazima NAY angekimbilia kujinasibu upande wa kujimudu kiuchumi mahali ambapo youngkiller anaona amezidiwa na nay wa mitego.
“Nimesema sina hela kwa sababu ujue tunazidiana kifedha n.k, na Nay ni mtu ambaye kiuhalisia anaonekana kanizidi vitu vingi kuhusiana na uchumi, kwa hiyo niliamini kabisa point yake kubwa itakuja umenijibu, lakini wewe huna hela ya kunizidi,wewe ni kapuku kwa hiyo ile ilikuwa ni kwake,kuwa hana kingine cha kunizidi,zaidi ya hela” ameiambia Ladha 3600 ya E FM na kuongeza.
“Nataka tuje kimichano, tupeane kimichano, toa facts nitoe facts, toa point eeh bhana Young Killer muziki wako unaharibika kwa sababu ya hivi na hivi na mimi nitoe facts za wewe kuporomoka kimuziki,” amesema Young Killer.
Wasanii hawa wamekuwa na mvutano mara baada ya Nay wa Mitego kumchana  Young Killer katika ngoma yake ‘Moto’ lakini alikuja kujibiwa kutipitia ngoma ya True Boya ya dogo youngkiller.

BONGO FLASH: NUH MZIWANDA AFANYIWA UPASUAJI WA SHINGO>>>>>

Hit maker wa Jike Shupa,Anameremeta n.k Nuh Mziwanda amewashukuru wahudumu wa hospitali ya Mwananyala kwa kunifanyia upasuaji salama.
Muimbaji huyo amedai amefanyiwa upasuaji wa shingo baada ya kupata maumivu makali sana shingoni.
“Thanks Jesus ’thanks MY SUPER DR KIWALE BINGWA kabisa wa upasuaji ‘Na MWANANYAMALA HOSPITAL kwa surgery (Upasuaji)uliokua chini ya shingo yangu’ bila kusahau MAMA yangu,mke wangu na ndugu zangu waliokua pamoja na mimi.naomba Maombi yenu Mashabiki wangu nirudi katika hali yangu na Kazi ziendelee.I Love you,” aliandika Nuh Instagram.
Hata hivyo haijajulikana mara moja alikuwa anasumbuliwa na nini.