Friday, July 7, 2017

BEEF JUU YA BEEF: NAY WA MITEGO HANA CHA KUNIZIDI ZAIDI YA HELA – YOUNG KILLER MSODOKI>>>

Msanii wa hip hop Bongo, Young Killer ametoa sababu ya kusema "hana hela" katika diss track ‘True Boya’ aliyoiachia kwa ajili ya Nay wa Mitego.Rapper huyo ameeleza kuwa aliamini baada ya kumjibu Nay kupitia ngoma hiyo ni lazima NAY angekimbilia kujinasibu upande wa kujimudu kiuchumi mahali ambapo youngkiller anaona amezidiwa na nay wa mitego.
“Nimesema sina hela kwa sababu ujue tunazidiana kifedha n.k, na Nay ni mtu ambaye kiuhalisia anaonekana kanizidi vitu vingi kuhusiana na uchumi, kwa hiyo niliamini kabisa point yake kubwa itakuja umenijibu, lakini wewe huna hela ya kunizidi,wewe ni kapuku kwa hiyo ile ilikuwa ni kwake,kuwa hana kingine cha kunizidi,zaidi ya hela” ameiambia Ladha 3600 ya E FM na kuongeza.
“Nataka tuje kimichano, tupeane kimichano, toa facts nitoe facts, toa point eeh bhana Young Killer muziki wako unaharibika kwa sababu ya hivi na hivi na mimi nitoe facts za wewe kuporomoka kimuziki,” amesema Young Killer.
Wasanii hawa wamekuwa na mvutano mara baada ya Nay wa Mitego kumchana  Young Killer katika ngoma yake ‘Moto’ lakini alikuja kujibiwa kutipitia ngoma ya True Boya ya dogo youngkiller.

No comments:

Post a Comment