Sunday, December 4, 2016

RAIS WA TANZANIA DKT.JOHN MAGUFULI,AMEELEZEA KUSIKITISHWA KWAKE NA TAARIFA ZA UZUSHI,KUWA AMEZUIA MIZIGO YA MRS KIKWETE,ISIINGIZWE NCHINI KUWA INAKWEPA KODI>>>

MHESHIMIWA DKT JOHN POMBE MAGUFULI
RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
RAIS Dk. John Pombe Magufuli ameeleza kusikitishwa kwake na uzushi unaofanywa kwa lengo la kumchafua Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete na familia yake huku na yeye akihusishwa na kuwataka wote wanaoeneza uzushi huo kuacha mara moja.
Rais Magufuli ameyasema hayo baada ya siku za karibuni vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuchapisha taarifa zinazomhusisha Mama Salma Kikwete na taasisi anayoiongoza ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) kwamba imeshindwa kulipia kodi mizigo mikubwa iliyoingizwa nchini na hivyo kuwa hatarini kupigwa mnada huku Rais Dkt. Magufuli akihusishwa kuzuia mizigo hiyo mpaka hapo itakapolipiwa kodi.

Soma taarifa kamili hapa chini;

No comments:

Post a Comment