Monday, November 21, 2016

PICHA 5: MCHUNGAJI ANAYEOMBEA WATU NA KUWAPULIZIA DAWA YA MBU..>>>>>>>


taarifa hii inaweza kukushtua sana, imetokea nchini Afrika Kusini kumuhusu mchungaji  Lethebo Rabalago wa Kanisa la Mountzion General Assembly lililopo mji wa Limpopo, ambaye amekutwa akiwapulizia dawa ya kuua wadudu kwa madai kwamba itawaponya matatizo yao.
Kupitia picha alizozishare kwenye ukurasa wake wa Facebook, ameonekana akiwapulizia dawa hizo waumini kwenye sehemu mbalimbali za mwili na kueleza kwamba yeye kwake kila kitu anaweza kukifanya kuwa baraka za uponyaji.
Sasa muda mfupi baada ya kusambaa kwa taarifa na picha za Mchungaji huyo akitumia dawa ya kuua wadudu kuwapulizia waumini kanisani kwake, Kampuni inayotengeneza dawa hizo iitwayo Doom imetoa tamko lake na kumuonya mchungaji huyo kuacha mara moja kutumia bidhaa zake kwa matumizi ya aina hiyo.
Na tayari imetoka taarifa kuwa vyombo vya usalama nchini Afrika Kusini vimeanza uchunguzi juu ya tukio hilo la mchungaji.

HIZI NI PICHA ZAIDI ZA NDUGU HUYO....
 
"ukistaajabu ya musa,utayaona ya firauni"
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment