Saturday, November 19, 2016

BUSU LA JENIFER LOPEZ LAHARIBU NDOA YA MUMEWE WA ZAMANI MARC ANTONY NA MPENZI MPYA WA ANTONY,SHANNON DE LIMA>>>>

MARC ANTONY WITH SHANNON DE LIMA
VYANZO vya habari vya E! News na Us Weekly vimeripoti kwamba, ndoa ya mwimbaji maarufu duniani, Marco Antonio Muñiz ‘Marc Anthony’ (48) ametengana na mkewe ambaye ni model kutoka nchini Venezuela, Shannon De Lima (28) chanzo kikitajwa kuwa ni msanii mwenzao Jennifer Lopez.Wapenzi hao waliodumu kwenye ndoa yao kwa miaka miwili tangu mwaka 2014, wameachana hivi karibuni huku chanzo kikielezwa kuwa, siku ya Usiku wa Tuzo za 17 za Latin Grammy Awards, wakati Marc Anthony akitumbuiza, ghafla mkewe wa zamani alipanda jukwaani na kumbusu mumewe huyo wa zamani jambo ambalo lilimtia wivu na limemkasilisha Shannon De Lima mpaka kufikia hatua ya kuchukua uamuzi wa kutengana na mumewe huyo.
JENIFER LOPEZ AKIBUSIANA NA MUMEWE WA ZAMANI THE LEGEND MARC ANTONY
Anthony ambaye usiku huo alinyakuwa tuzo ya Person of the Year amejitetea na kusema kuwa, alichokifanya kwa Lopez ni sawa na kumbusu ‘dada yake’. Meneja wa Lopez Benny Medina, yeye amesema kuwa wawili hao ambao wamezaa watoto mapacha wawili hawajarudiana kamwe.
Mbali na kumbusu, Lopez alimpa maneno matamu Anthony usiku huo wa Alhamisi. 
“Marc, you are a living legend who has laid bare your heart and soul on your musical journey,” she said in Spanish. “We’ve learned so much and we’ve grown so much, and you’ve always been so many things in my life: my mentor, a twin soul, a father who’s not only the person of the year, he’s the person of all time.”
Anthony alitoa pongezi kwa watoto wake watano na kusema “all those people who told me I would never make it.” Japo hakumtaja mkewe De Lima.
Anthony na De Lima walianza mahusiano Januari 2012, miezi saba baadaye Anthony na aliyekuwa mkewe kipindi hicho Lopez walitangaza kwa pamoja kuwa na mpango wa kuachana.
Baada ya kuachana huko, Januari 2013, Anthony na De Lima waliamua kuoana na kufunga ndoa kimya kimya huko Jamhuri ya Dominican mnamo November 2014. Hawajajaliwa kupata watoto wa pamoja.
 
UNGANA NAMI KUPITIA ===>FACEBOOK>>>>>
 
 

No comments:

Post a Comment