Sunday, November 20, 2016

REPORT KUTOKA WASAFI LABEL,JUU YA AMBER ROSE,STAA MKUBWA WA MAREKANI>>>>>>

Katika kusheherekea Christmas mwaka huu, label mahiri Tanzania yenye wasanii wakali na producer mzuri ya WCB wanatarajia kufanya show yao ya kwanza wakiwa pamoja, December 24 iliyopewa jina Wasafi Beach Party jijini Dar es Salaam.
Wasanii wote wa label hiyo wakiongozwa na Diamond platnumz watatumbuiza. Lakini huenda kukawa na ugeni mkubwa wa staa wa nje na tayari meneja wa Diamond, Sallam amedeclare jina.
Akiweka picha ya mrembo wa Marekani, Amber Rose, Sallam ameandika kwenye Instagram, “watu Wangapi wanataka huyu dada ashuke bongo siku akinukishe watu wale nae Bata???”
Nae Diamond alichombeza kwenye post yake: Eti Manager @sallam_sk anauliza wangapi wangependa huyu dada @amberrose siku ashuke Bongo watu wale nae Bata???”
Huenda label hiyo ikawa imepanga kumleta mrembo huyo kuwa host wa tamasha lenyewe.
Hiyo haitakuwa mara ya kwanza kwa ex huyo wa Wiz Khalifa kuja Afrika japo itakuwa mara ya kwanza kushuka bongo. Mwaka jana alienda Lagos, Nigeria kwa mwaliko wa D’Banj ambako hata hivyo alikaa jukwaani kwa dakika 7 tu.
diamond platnumz,MWANAMUZIKI MASHUHURI AFRICA,W.C.B-OWNER
 
utanipenda? the best song and video from diamond platnumz

 

No comments:

Post a Comment