Wednesday, October 26, 2016

HII NI KAULI YA MKUU WA CHUO CHA DAR ES SALAAM(UDSM) RAIS MSTAAFU MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE,ILIYOIBUA MIJADALA MBALIMBALI KWENYE MITANDAO NA MAGAZETI WIKI HII>>>>>>

MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE
RAIS MSTAAFU WA TANZANIA
MKUU WA CHUO KIKUU UDSM
story kamili by JULIE KAVISHE-JOURNALIST MACHAS BLOG
Kauli ya Rais Mstaafu, Dk Jakaya Mrisho Kikwete imemfanya aingie kwenye vichwa vya habari wiki hii. kauli hiyo ambayo Aliitoa wakati akihutubia mbele ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 55 ya chuo hicho, katika sehemu ya hotuba yake alisikika akisema, “Ukiwa mpya lazima watu waone una mambo mapya, lakini mapya ya maendeleo, aliisema kauli hiyo huku akiangalia hadhira inayomtazama huku akitabasamu.aliongeza kwa kusema:-
“Sio mapya ya kubomoa  kule tulikotoka,” aliongeza kwa kicheko na kuendelea na hotuba yake.
Bado haijaweza kufahamika kauli yake ilimaanisha nini. Kikwete ni Mkuu wa chuo kikuu hicho.
 
>>>>>>>>>>>RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE,ANAFAHAMIKA KAMA MZEE WA MADONGO NA MISEMO,NI MTU MASHUHURI KWENYE KAULI MBALIMBALI KILA ANAPOZITOA.
 
"TAFASIRI JUU YA MISEMO YAKE HIYO IPO AKILINI MWAKE,JAPO PIA WEWE KAMA WEWE UNAWEZA KUNYUMBUA NA KUTAFSIRI KIMTAZAMO" #TAFAKARI
 
 

No comments:

Post a Comment