Tuesday, April 5, 2016

MATAJIRI 50 WANAOONGOZA BARANI AFRICA.....

 

TAJIRI NAMBA MOJA AFRICA, ndugu,ALIKO DANGOTE

 

Kwa ufupi

Kwa mujibu wa jarida maarufu la Forbes linalofuatilia kwa karibu watu
maarufu, lililotolewa wiki iliyopita, mabilionea wapya wamepungua kutoka 28 mwaka jana hadi 23 mwaka 2015
Kudorora kwa uchumi katika baadhi ya nchi za Afrika, kumesababisha kupungua kwa idadi ya mabilionea wapya walioingia kwenye orodha ya 50 bora mwaka huu.
Kwa mujibu wa jarida maarufu la Forbes linalofuatilia kwa karibu watu
maarufu, lililotolewa wiki iliyopita, mabilionea wapya wamepungua kutoka 28 mwaka jana hadi 23 mwaka huu.
Kudorora kwa bei ya bidhaa mbalimbali kwenye soko la dunia kumetajwa kuwa sababu ya hali hiyo.
Jarida hilo linaeleza kuwa mabilionea wote 50 liliowaorodhesha wanautajiri wa dola 95.6 bilioni (Sh250 trilioni).
Mapato hayo yameshuka kwa Sh32.2 trilioni ikilinganishwa na mwaka jana. Katika orodha hiyo, Aliko Dangote kutoka Nigeria ndiye anayeendelea kushikilia nafasi ya kwanza kwa mwaka wa tano mfululizo akiwa na utajiri wa dola 16bilioni (Sh34.4 trilioni), ukiwa umepungua kwa Sh10.7 trilioni ikilinganishwa na mwaka jana.
Forbes inataja kuzorota kwa mapato katika viwanda vya saruji anavyovimiliki tajiri huyo katika nchi mbalimbali za Afrika kuwa ndiyo sababu ya kushuka kwa kiwango cha kwa utajiri wake. Pia, sababu nyingine ni kushuka thamani kwa fedha ya Nigeria, Naira.
Mabilionea wengine katika orodha hiyo ni Nicky Oppenheimer, aliyeshika nafasi ya pili akiwa na utajiri wa dola 6.6bilioni (Sh14.1 trilioni) zilizopatikana kutokana na biashara ya uchimbaji na
uuzaji dhahabu.
Oppenheimer alikuwa akishikilia namba tatu mwaka 2014, baada ya kuuza kampuni yake kubwa ya Debeer kwa kampuni ya Anglo American kwa dola 5.1bilioni (Sh10 trilioni) kabla ya mwaka huu kushika nafasi ya pili.
Christoffel Wiese anashika nafasi ya tatu akifuatiwa na Johann Rupert katika nafasi ya nne, akiwa na utajiri wa dola 6.5 bilioni (Sh13 trilioni), wengine na nafasi zao kwenye mabano ni King Mohammed VI (tano) akiwa na utajiri wa (Sh12.2 trilioni), Nassef Sawiris (sita) (Sh10 trilioni), Mike Adenuga (saba) (Sh7.5 trilioni), Isabel dos Santos (nane) (Sh7.5 trilioni), Issad Rebrab (tisa) (Sh6.8 trilioni) na Naguib Sawiris aliyeshika namba 10 akiwa na utajiri wa Sh6.4 trilioni.
Katika orodha hiyo ya mabilionea, Afrika Kusini ndiyo yenye matajiri wengi zaidi ikiwa nao 16 kwa miaka kumi na moja mfululizo huku Nigeria ikifuatia kwa kuwa na mabilionea 10 pekee kutoka 13 iliyowahi kuwa nao miaka ya nyuma.
Morocco nayo inafanya vizuri katika orodha hiyo ikiwa na mabilionea wanane, Misri (saba), Tanzania (watatu), Kenya (watatu) na bilionea mmoja kutoka Algeria, Angola na Uganda.
Pia, katika orodha hiyo bilionea aliyeingia kwa mara ya kwanza kutoka Kenya ni Narendra Raval ambaye ana utajiri wa Sh860 bilioni. Raval ni mhubiri wa zamani wa madhehebu ya Kihindu katika hekalu la Swaminarayan.
Anadaiwa kuvuliwa cheo chake baada ya kumuoa mwanamke raia wa Kenya. Baadaye alijiingiza katika biashara ya kutengeneza vyuma kisha akafungua kampuni ya Devki Group inayouza saruji, nondo na nyaya.
Kwa upande wa wanawake, orodha hiyo inaonyesha kuwapo kwa wanawake wawili ambao mara kadhaa wamekuwa wakijitokeza katika kundi hilo.
Isabel dos Santos wa Angola na Folorunsho Alakija wa Nigeria.
Dosantos ni mtoto mkubwa wa Rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos. Mwanamke huyo amewahi kuchunguzwa na Bunge la Ulaya kutoka na uwekezaji mkubwa alioufanya nchini Ureno hasa baada ya kununua kampuni inayojishughulisha na usambazaji vifaa vya umeme ya Efacec Power Solutions kwa Sh430 bilioni.
Mmoja wa wabunge wa Bunge la Ulaya, alitoa hoja ya kutaka mwanamke huyo kuchunguzwa kwa madai kuwa upo uwezekano mkubwa wa kutumiwa vibaya fedha za Serikali ya Angola.
Watanzani watatu wajitokeza
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (Metl), Mohammed Dewji (40), ndiye aliyetajwa kuwa bilionea mdogo zaidi katika orodha hiyo akiwa na utajiri wa Sh2.3 trilioni huku akishikilia namba 21 kati ya mabilionea 50.
Dewji anaongoza kampuni ya Metl iliyoanzishwa na baba yake miaka ya 1970. Kampuni hiyo inamiliki viwanda vya nguo, unga, vinywaji na mafuta ya chakula.
Mtanzania anayefuata katika orodha hiyo ni mfanyabiashara Rostam Aziz anashika nafasi ya 25 akiwa na utajiri wa dola Sh1.9trilioni.
------> Mtanzania mwingine kwenye orodha hiyo ni Said Salim Bakhresa aliyeshika nafasi ya 36 Afrika akiwa na utajiri wa Sh1.2 trilioni.
Pia, katika orodha hiyo, Miloud Chaabi (86) kutoka Morocco ametajwa kuwa ndiye bilionea mzee kuliko wote Afrika. Mzee huyo anamiliki kampuni inayojihusisha na ujenzi wa nyumba za makazi na biashara. Vilevile, ana hisa nyingi katika kampuni ya kutengeneza kemikali.
Utaratibu uliotumika
Moja ya vigezo vinavyotumiwa na Forbes kuwafahamu mabilionea wa Afrika ni aina ya uraia wa mtu husika. Kwa mfano, bilionea Mo Ibrahim, anayefahamika kuwa Mwafrika kutoka Sudan, ameshindwa kuingizwa kwenye orodha hiyo baada ya kuchukua uraia wa Uingereza.
Pia, jarida hilo, linakokotoa utajri wa mtu kwa kuangalia thamani ya mali anayomiliki mtu ilivyo sokoni wakati ikifanya tathmini hiyo.
Kwa mfano, katika orodha hiyo, ilitumia thamani ya fedha ilivyokuwa mwishoni mwa wiki ya Novemba 13.
Vilevile, Forbes limekuwa likikwepa kuzifanyia thamani mali zinazomilikiwa na familia ambazo mchanganuo wake haueleweki.     

No comments:

Post a Comment