Sunday, October 23, 2016

CALISAH,AMBAE ANATAJWA KUWA NA MAHUSIANO NA WEMA SEPETU,AMETAMKA KUWA ETI HAMTAMBUI THE BIGGEST BIG BROTHER AFRICA STAR IDRIS SULTAN,JE NI KWELI HAMFAHAMU STAR HUYU WA BIG BROTHER?

CALISAH,MODO KUTOKA TANZANIA.
Model anayedaiwa kutoka kimapenzi na staa wa filamu NCHINI TANZANIA, Wema Sepetu, Calisah amefunguka na kuzungumzia tetesi hizo ambazo zimekuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii.
Kijana huyo ambaye tayari ameshaonekana mara kadhaa katika baadhi ya video za mastaa wa muziki nchini, amemmwagia sifa malkia huyo wa filamu huku akishindwa kuweka wazi kama ni kweli anatoka naye kimapenzi au la!.
“Wema is a beautiful girl, sexy and every man’s dream, na mimi pia ni mvulana mzuri ambaye mwanamke yeyote angependa kuwa na mimi, akiwemo Wema mwenyewe,” Calisah alikiambia kipindi cha FRIDAY NIGHT LIVE cha EATV. “Siwezi kusema moja kwa moja kwamba sisi ni wapenzi, lakini lazima ujue kuwa Wema ni mzuri na mimi ni mzuri,”
Pia kijana huyo alidai kuwa hamtambui Idris Sultan na hakumbuki kama Tanzania imewahi kuwakilishwa na mtu anayeitwa Idriss katika mashindano ya Big Brother Afrika.
“Who? Idriss, kwani amewahi kuwa Big Brother? Which year?,” aliuliza kijana huyo.
Malkia huyo wa filamu toka aachane ama atengane na mshindi huyo, the biggest celeb in africa #Big Brother Afrika 2014, hajaweka wazi mahusiano yake mapya.
AT FRIDAY NIGHT LIVE 21ST OCTOBER 2016
IDRIS SULTAN-BIG BROTHER AFRICA WINNER 2014
WEMA ISACK SEPETU-MUIGIZAJI WA FILAMU NCHINI TANZANIA
 
"HAYO NDIO MAISHA YA UMAARUFU"
 
 

No comments:

Post a Comment