Thursday, September 15, 2016

MHESHIMIWA TUNDU ANTPASI MUGHWAI LISSU: SERIKALI ISITUMIE FEDHA ZA HIFADHI YA MIFUKO YA JAMII KANA KWAMBA NI ZA KWAKE,NA HATIMAE KUACHA KUZIRUDISHA >>>>>

HON. TUNDU LISSU,MP IKUNGI SINGIDA,EXECUTIVE LAWYER (CHADEMA)
 
----tundu lissu anaandika....
Pesa za mifuko ya hifadhi ya jamii hazitajenga kiwanda chochote. Ni siasa tu.
Pesa za mifuko ya hifadhi ya umma sio pesa za serikali, ni pesa za wafanyakazi. Zinatokana na makato yao ya mishahara.

Serikali imekuwa inatumia pesa hizi kama zake, wakati sio zake. Pesa hizo zimetumika kujenga UDOM kwa makubaliano kwamba serikali hii ingerudisha pesa hizo kwa mifuko hiyo. Haijarudisha hata senti moja.

Pesa hizo zimejenga jengo la Usalama wa Taifa OysterBay Dar. Serikali haijarudisha hata senti moja kwa mifuko ilikochota pesa hizo. Pesa za mifuko zimejenga jengo la Machinga Complex Ilala Dar na nyumba za polisi Kurasini Dar. Serikali haijarudisha hata senti moja. Ndizo zilizojenga Daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni. You can rest assured haitarudi hata senti moja.
Ukweli, kama alivyosema CAG kwenye mojawapo ya taarifa zake za mwaka, mifuko ya hifadhi ya jamii ina hali mbaya ya kifedha. Hii ndio sababu wenye mamlaka wanataka kuondoa fao la kujitoa. Wameigeuza mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa shamba la bibi mpaka mifuko inakaribia kufilisika.

Sasa wanataka kuficha uchafu huu kwa blangeti la uzalendo uchwara. Wafanyakazi wa Tanzania wakikubali udanganyifu huu wataliwa kama ambavyo pesa zao zimeliwa kwenye miradi niliyoitaja.
Suala sio tuache siasa. Hatuwezi kuacha siasa. Suala ni tuache siasa za aina gani. Hawa wanasiasa wanaojivika uzalendo uchwara kuhusu hela za wafanyakazi wao wenyewe wametengenezewa utaratibu maalum ambapo wanakatwa na NSSF halafu baada ya kumaliza ubunge wanarudishiwa pesa zao. Hawasubiri wafikishe miaka sitini ndipo wapate mafao yao ya kujitoa.

Halafu wanawahubiria wafanyakazi wasubiri miaka sitini ndipo wapate mafao yao. Wana ndimi mbili kama za nyoka. Wafanyakazi wa Tanzania amkeni, hamna chochote cha kupoteza isipokuwa minyororo yenu.

Soure:Henry Kilewo

No comments:

Post a Comment