Thursday, August 4, 2016

WASANII MAARUFU NCHINI TANZANIA UDEUDE(MTUNZI NA MWIMBAJI) NA IQU JUNIOR WAFARIKI DUNIA......

 
***Msanii na mtunzi wa nyimbo za Bongo Flava, Hamid Hafidh maarufu kama Ude Ude na rafiki yake Iku wameuawa katika tukio la ujambazi mkoani Tanga.
 
Ude Ude enzi za uhai wake
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi wawili hao walikuwa miongoni mwa majambazi wanne waliokuwa na gari aina ya Toyota Probox waliokurupushwa na polisi katika jaribio la kuiba vifaa vya magari ya halmashauri.
Tukio hilo lilitokea jana saa mbili asubuhi walipokutwa wakivunja gari la mwalimu wa shule ya sekondari, Maweni aliyejulikana kwa jina la Dominica Tarimo.
Wananchi wakiwa na piki piki na magari pia waliungana na polisi kuwafukuza watu hao na kuwashambulia.

Miili ya wasanii hao baada ya kuuawa
Polisi wamedai kuwa watu hao walijihami na silaha zenye ncha kali ili kujiokoa na wawili kupiga risasi huku wawili wakitokomea kwenye msitu ulio jirani na kiwanda cha saruji cha Sungura.


*********Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga, Leonard Paul amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

UDEUDE(KUSHOTO) NA IQU JUNIOR(KULIA) ENZI ZA UHAI WAO
 
VIDEO WIMBO WA IQU JUNIOR FT ALIKIBA "NISAMEHE"
 
Marehemu Ude Ude alijipatia umaarufu kwenye muziki wa Bongo Flava kwa umahiri wake wa utunzi kwa kuwaandikia nyimbo wasanii mbalimbali. Nyimbo alizozitunga ni pamoja na ‘Wangu’ wa Lady Jaydee, ‘Maneno Maneno’ wa Queen Darleen, Ulofa by Top C, ‘Bwashee’ ya Baby J, ‘Oyoyo’ ya Bob Junior na zingine kibao. Wimbo wake ulioweza kuhit ni Ngoma Inogile – waweza kuangalia video yake hapo chini.
 
HERE IS THE VIDEO CALLED "NGOMA INOGILE" BY #UDEUDE
 
Wasanii mbalimbali wametoa salamu zao za rambi rambi kwa msiba huo akiwemo Z-Anto aliyeandika:
"Miongon mwa vtu vbaya katka maisha ya binadam ni kuisema maiti, hakuna ajuae mwisho wake hakuna ajuae chanzo cha umauti wake, waweza kuwa mcha mungu lakin chanzo cha umauti wako ikawa ni zinaa, au uongo, ama wizi, ama utapeli, ama lolote ambalo hukuwah kulifanya ama kulitarajia ndio maana tunaambiwa ktk vtabu vyetu tunapaswa kujiombea kupata mwisho mwema, wangap walikuwa ni wenye dhambi hawamjui mungu wao pengne walikuwa vchochez wa vtu vbaya lakin nia zao za mwisho zkawafanya wapate mwisho mzur wa maisha yao kama watu waliofariki makka walipokwenda kuhiji, so tusipoteze muda kuzisema maiti kwan cc pia ni maiti watarajiwa na hatujui mwisho wetu, tusemeni, inna lillah wainna ilaih Rrajiuun/bwana ametoa na bwana akatwaa"

SOURCES:

MWANANCHI

jamii forums

bongo 5

by MACHAS OFFICIAL SITE

 

No comments:

Post a Comment