Wednesday, August 31, 2016

TCRA KUWANYOOSHA WATU MIAKA 20 JELA ,WANAOWEKA PICHA ZA NUSU UTUPU/UTUPU WENYEWE MITANDAONI...

Unataka kwenda jela? Ni rahisi sana, weka picha za ngono mtandaoni, hatimae utakuwa mkazi wa huko kwa kipindi cha miaka 20.

Kwa mara nyingine tena, mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA imewakumbusha watanzania kutochezea sheria za mitandaoni lasivyo wataingia  pabaya.

“Ni vyema wananchi wakatambua kwamba uchochezi kwenye mitandao kwa kusambaza ujumbe wenye viashiria vya uvunjifu wa amani au kuweka picha zisizofaa kwenye mitandao sheria ipo wazi na watu watajikuta wanaishia pabaya, hivyo ni vyema kuchukua tahadhari mapema,” alisema Mhandisi wa Mawasiliano wa TCRA Victoria Rulakara wakati akizungumza kwenye kipindi cha Hotmix cha EATV.
Wakati huo huo, mamlaka hiyo imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ikiwa ni pamoja na kuwaonya watu wanaonzisha blog zenye majina ya uongo kutukana watu wengine.

Sheria ya Makosa ya Mitandaoni ilipitishwa mwaka jana 2015 na rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete.

#MACHAS OFFICIAL SITE

No comments:

Post a Comment