Wednesday, August 24, 2016

BELLE 9, KUJIUNGA WCB????????????????????

BELLE 9,MSANII MAHIRI WA MUZIKI R&B KUTOKA TANZANIA
Baada ya vocalist, Rich Mavoko kusaini WCB ya Diamond, huwenda msanii wa muziki wa R&B kutoka Morogoro, Belle 9 na yeye akasaini ndani ya label hiyo.

Muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo wake ‘Bugger Movie Selfie’ ameonekana akifanya mazoezi na bendi ya Diamond katika ofisi za WCB.

Kwa mujibu wa kipindi cha Planet Bongo cha EATV, Belle 9 pamoja na Diamond wameonekana wakiimba wimbo ‘Mdogo Mdogo’ kwa pamoja huku wakicheza.

Hatua hiyo imefufua matumaini mapya kwa mashabiki wa muziki kuona huwenda WCB ikamsaini msanii huyo kama ilivyofanya kwa Rich Mavoko.
Kwa sasa label ya WCB ina wasanii wanne, Harmonize, Rich Mavoko, Raymond aka Rayvany pamoja Queen Darlin.
 
#MACHAS OFFICIAL SITE

No comments:

Post a Comment