Monday, October 31, 2016

PICHA 19:MSHINDI WA MAISHA PLUS(MAISHA HALISI YA KIJIJINI) EAST AFRICA 2016,SHINDANO AMBALO LILIANZISHWA MNAMO MWAKA 2009>>>>>

Olive Kiarie, mshiriki kutoka nchini Kenya ameibuka mshindi wa Maisha Plus East Africa 2016 na kujishindia kitita cha Tzshs. Milioni 30.Shukrani zake baada ya kutangazwa kushinda"Kwanza napenda kumshukuru Mungu. Nimetoka Kenya kuja kutafuta hii pesa na nimeipata, hivyo namshukuru Mungu. Nawashukuru mabeste wangu wote, na wote walionipa sapoti. Asante pia Babu.”
OLIVE KIARIE,AKILIA KWA FURAHA
Hii ni mara ya kwanza kwa taji hilo kwenda nje ya Tanzania ikiwa ni msimu wa tano toka mashindano haya yaanze mwaka 2009. Olive anakua msichana wa pili kujishindia taji hilo baada ya Bernick Kimiro aliyeshinda mwaka 2012.Shindano la Maisha Plus lilijumuisha washiriki 30 kutoka nchi tano za Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda ambapo washiriki 16 tu ndio waliofanikiwa kuingia fainali.Washiriki Aloyce Sambuta, Irene Ishengoma, Alex Essau, Ngenda Pilly, Nibigira Baswari, Grace Pemba, Denaice Machocho, Umubyeyi Solange, Assimwe Marvin, Salmin Omary, Rukia Athuman, Mike Curtywer, Yasinta Mrisho, Karekezi Jean na Namita Cherrie walifanikiwa kuingia fainali ambazo zilirushwa juzi usiku na kituo cha televisheni cha Azam Two.Katika hatua nyingine washiriki wanne walipewa tuzo. Aloyce Sambuta alipata tuzo ya Rais bora na kupewa jumla ya Tshs.Laki nne, Ngenda Pili alipata tuzo ya mshiriki mwenye heshima kubwa, Mike Cutywer alipaza tuzo ya mshiriki mdogo wa kiume wakati Namita Cherrie alipata tuzo ya mshiriki mdogo wa kike.Wasanii Ommy Dimpoz na Joh Makini walitoa burudani wakati wa fainali hizo.
Washiriki walioingia Top 5 ya Maisha Plus kutoka kushoto: Aloyce Sambuta, Alex Essau, Olive Kiarie, Irene Ishengoma na Ngenda Pilly.
Top 3 ya Maisha Plus Aloyce Sambuta, Olive Kiarie na Irene Ishongoma
C.E.O & CO-ORDINATOR WA SHINDANO NDUGU MASOUD KIPANYA,AKIZUNGUMZA JAMBO,KULIA NI BONGOFLEVA ARTIST OMMY-DIMPOZ
HIP-HOP STAR TANZANIA, JOH-MAKINI AKIPERFORM KWENYE SHINDANO HILO
MASOUD KIPANYA AKITETA JAMBO NA JOH MAKINI
MGENI MUALIKWA,AKIMTANGAZA MSHINDI
OLIVE KIARIE,AKISHANGAA MARA BAADA YA KUTANGAZWA KUWA NDIYE MSHINDI WA SHINDANO HILO
AKIPONGEZWA NA WASHIRIKI WENZAKE
MGENI MUALIKWA,MSHINDI NA BABU WA KIJIJI
AKIPONGEZWA NA WASHIRIKI WENZAKE
PICHA YA PAMOJA NA LOGO.
WANAWAKE MBALIMBALI KUTOKA KENYA WAKIFURAHIA USHINDI KWENDA KWAO
KUTOKA KULIA NI MSHINDI WA MAISHA PLUS 2012,BERNICK KIMIRO,PAMOJA NA MSHINDI WA 2016 MAISHA PLUS EAST AFRICA,OLIVE KIARIE.
 
PREPARED & EDITED BY

No comments:

Post a Comment