Monday, April 3, 2017

KIUKWELI NIMEJISIKIA POA SANA BAADA YA DIAMOND KUIKUBALI MISTARI KADHAA YA NYIMBO ZANGU,HADI KUITUPIA INSTAGRAM-YOUNG KILLER"MSODOKI">>>

Diamond Platnumz ni shabiki mkubwa wa Young Killer. hitmaker huyo wa ‘Marry You’ si mtu anayesikiliza nyimbo za Msodoki juu juu tu, bali kwa undani kiasi cha kushika mistari kadhaa.
Mwishoni mwa wiki, Diamond alionesha wazi kuzimia mistari konde ya rapper huyo wa Mwanza kwa kuandika minne kwenye post zake nne tofauti za Instagram na Twitter.
Mistari ya Young Killer ambayo Diamond ameiandika kwenye post zake za Instagram ni pamoja na:
1. Asa Unataka kuwa mimi na mimi ntakuwa nani….? (Sinaga Swagga (Part1)
2. Naskia Usingizi ni Mbolea ndiomaana tukilala tunaota…? (Sinaga Swaga Remix)
3. Ukiona Nina changamoto changa Unga tusonge Ugali… Mwisho wa siku wote tunashiba, na Mambo yanakuwa shwari (Sinaga Swagga 1)
4. Shida ingekuwa sumu basi tungekufa wengine (Kumekucha f/ Mr Blue)
“Binafsi nafarijika sababu [Diamond] ni mtu ambaye ana fan base kubwa kwahiyo anapokuwa ameshow love kwa kitu kama hicho kupost mistari yangu hata mashabiki wake pia wanakuwa wananiamini kuwa Young Killer anafanya kazi nzuri,” rapper huyo alipokuwa akizungumza na reporter wa blog hii.
“Kwahiyo ni moja kati ya msaada, sio lazima akulipie video, akupeleke studio ukarekodi, ni kitu chochote anachoweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine.”aliongeza rapper huyo mdogo mwenye jina kubwa bongo...

bado nakukumbusha kuwa,usipite bila kupitia youtube chanel yetu kwa taarifa,burudani na matukio kadha wa kadha,pia usiache kusubscribe ili uwe wa kwanza kupata access SUBSCRIBE TO OUR YOUTUBE CHANEL

No comments:

Post a Comment