Tuesday, April 11, 2017

CCM ACHENI UNAFIKI,KUHUSU UTEKWAJI WA WATU,NIPO TAYARI HATA NIFUKUZWE KWENYE CHAMA-HUSSEIN BASHE>>>>

MHESHIMIWA HUSSEIN BASHE
MBUNGE WA NZEGA MJINI(TABORA)
Mbunge wa Nzega Mjini(CCM) Hussein Bashe amewataka wabunge wa CCM kuacha unafiki kuhusu suala la watekaji watu huku akisema kuwa yeye ni mmoja wa watu waliokamatwa na usalama wa Taifa(TISS).
Bashe ameyasema hayo Jumanne hii leo bungeni mjini Dodoma.
“CCM acheni unafiki mimi nimeshakamatwa na watu wa usalama mnasema hawakamati, kwa hili nipo tayari mniondoe kwenye chama”,amesema Bashe
Bashe alikuja juu baada Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene kumtaka Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kuthibitisha kuwa matukio ya ukamataji na utekwaji wa watu yanafanywa na usalama wa Taifa.....
bado nakukumbusha kuwa,usipite bila kupitia youtube chanel yetu kwa taarifa,burudani na matukio kadha wa kadha,pia usiache kusubscribe ili uwe wa kwanza kupata access SUBSCRIBE TO OUR YOUTUBE CHANNEL

No comments:

Post a Comment