Saturday, March 25, 2017

UTAALAMU:WANASAYANSI WAGUNDUA KUTENGENEZA DAMU KUPITIA MAABARA,ITAUZWA BEI GHALI(HIGH EXPENSIVE RATE)>>>>

BLOOD TYPES/CATEGORIES
Wanasayansi wanasema kuwa wamepiga hatua kubwa katika uzalishaji wa damu yenye seli nyekundu kwa wingi itakayotumiwa kuwasaidia wagonjwa.Seli yekundu hutengezwa katika maabara lakini tatizo ni kiwango kinachohitajika.
Kundi moja la wanasayansi katika chuo kikuu cha Bristol-UK pamoja na idara ya damu na upandikizaji limetengeza mbinu ya kuzalisha kiwango kikubwa cha damu.
Damu hiyo ya maabara itakuwa bei ya juu ikilinganishwa na damu ya kawaida.
Kwa hivyo itatumiwa miongoni mwa watu wasio na aina ya damu,YAAN WALE WASIO NA BLOOD TYPES MFANO-A,B,AB,O.
Mfumo wa zamani ulishirikisha kutumia kiini shina kinachotengeza seli nyekundu za damu katika mwili na kuzibembeleza kuzalisha seli kama hizo katika maabara.
Hatahivyo kila seli huchoka haraka na kushindwa kuzalisha zaidi ya seli nyekundu 50,000.
Mbinu iliyotengezwa na kundi hilo la wanasayansi wa Bristol inalenga kuzishika seli shina mapema wakati zinapokuwa kwa wingi.
Daktari Jay Frayne mmoja ya watafiti wa kundi hilo alisema: Tumeonyesha uwezo wetu wa kuzalisha seli nyekundu zinazoweza kutumiwa katika hospitali....
 

No comments:

Post a Comment