Friday, November 18, 2016

SHIRIKA LA NDEGE NCHINI RWANDA,[RWANDA AIR] LANUNUA NDEGE MPYA NZURI,KALI AFRIKA,LIKIWA NI SHIRIKA LA PILI DUNIANI KUNUNUA NDEGE YA AINA HII>>>>>>

BOEING 737-800
MOJA ya vitu ambavyo vina ‘kiki’ sana kwenye Mataifa ya Afrika Mashariki kwa sasa ni pamoja na huduma za usafiri wa anga, Shirika la Ndege la Rwanda, RwandAir limenunua ndege mpya aina ya Boeing 737-800 Next Gen ambayo inatarajiwa kuongeza ushindani wa safari za anga duniani.
RwandAir imekuwa kampuni ya kwanza Barani Afrika na ya pili duniani kununua ndege ya aina hiyo ambayo imewekwa vifaa vya kuwezesha abiria kutumia huduma za intaneti kwa njia ya Wi-Fi.
RWANDA AIRBUS 330-200
Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 154 ambapo ilitolewa oda ya kununuliwa na Rwanda miaka 6 iliyopita, imetua kwenye uwanja wa ndege wa Kigali Novemba 16, 2016 saa 10 usiku.
Waziri wa Uchukuzi wa Rwanda, dkt.Alexis Nzahabwanimana, amesema ndege hiyo mpya itawezesha shirika hilo kupanua safari zake barani Asia, Ulaya na Marekani.
Mwezi Septemba mwaka huu, Serikali ya Rwanda ilinunua ndege nyingine ambayo ni ya kwanza Afrika Mashariki aina ya Airbus 330-200, iliyopewa jina la ‘Ubumwe’ ikiwa na maana ya Umoja.
John Mirenge, Mkurugenzi Mtendaji wa RwandAir akiitambulisha ndege hiyo iliyopewa jina la ‘Kalisimbi’.
Dk. Alexis Nzahabwanimana, Waziri wa Usafirishaji akizungumza wakati wa mapokezi ya ndege hiyo.
 
"PONGEZI KWENU"
 
 

No comments:

Post a Comment