MHESHIMIWA.WILLIAM VANGIMEMBE LUKUVI
WAZIRI WA ARDHI,NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amesema atamchukulia hatua mfanyabiashara aliyemkabidhi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda eneo kwa ajili ya viwanda kwa sababu eneo hilo si lake ni mali ya Serikali.
Waziri Lukuvi ameyasema hayo Jumatatu hii katika mkutano wake na wanahabari. “Sitaki ardhi itumike kama sehemu ya wafanyabiashara kutakatishia fedha zao chafu,” amesema Lukuvi
Aidha Lukuvi amesema anataka watu wote wanaomiliki maeneo mijini kujisalimisha kwa maofisa ardhi wa wilaya kwa ajili ya uhakiki.
Chanzo: Mwananchi

No comments:
Post a Comment