IRENE UWOYA(TANZANIA ACTRESS,CCM-POLITICIAN)
Baada ya kashikashi za hapa na pale za wasanii wa bongo movie kuingia kwenye siasa huku Wema Sepetu akihamia CHADEMA na kusema anaidai CCM, swahiba wake, Batuli amekanusha. Wakati vita vya maneno vikiendelea, mwenzao, Irene Uwoya amewachana.
Irene ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika maneno au MAWAZO YAKE
Katika maisha siku zote ushauri unaruhusiwa kutolewa au kupokelewa… Lakin sio lazima mtu kupokea ushauri unaotolewa… Kila mtu anauhuru wakuamua kitu ambacho anahisi kinamfaa kwenye maisha sababu… Sazingine kwenye maisha Kuna sehemu inafika unacho jiskia kwenye moyo wako sio rahisi mtu mwingine kujiskia … Sasa ni mbaya sana kuishi kwa hisia… Ifikie Wakati tujitaidi kuheshimu hisia Za mtu… Lakin pia kunavitu vingine nazani Nivyema vkabaki kwa wausika wavinaowahusu…yani sio lazima kuongea kila kitu kwenye jamiii… Watu wanatamani sazingine kuskia vtu ambavyo wanahisi vinafaida kwa Jamii… Kunavitu vingine ukiongea havina maana.”
Mfano mim ni CCM damu… Lakin kunavitu vinaboa sanaaa Kiukweli kada mzima wa CCM unasimama hadharani unasema tulilipwa kufanya campaign? hatakama lakini unaifundisha Nin Jamiii? Unafundisha jamiii kwamba yote tuliyoongea kuhusu CCM hatukuwa tunamaanisha nikwasababu tulilipwa? Unaiambia jamiii ulikuwa tayari kuwadanganya na mliwadanganya sababu mlilipwa? Hivi Kweli? Kwahiyo jamiii ione Chochote Tutachoongea wasikiamini maana yake tutakuwa tumelipwa? Kwahiyo ata mnayoyaongea mnataka kusema mmelipwa? Mi-nazani tujifunze kunyamaza sazingine kama hamna ulazima wakuongea mnaweza kuhisi mnajenga kumbe mnaharibu kabisaaa… Embu Tufanye Kazi zinazo tuhusu Jamaniii… Nigeria wenzetu sasa wako Hollywood wanaigiza huko… Sisi ata nigeria kwenyewe bado hatuja pasua… Lakin hapa Tupo busy kushabikia ujinga na vitu vya kipumbafu na visivyo na Msaada kwajamiii… Kwastaili hiii… Hollywood tutaiskia na kuiona kwenye TV.
WEMA ISACK SEPETU-KADA MPYA WA CHADEMA,KUTOKEA CCM
No comments:
Post a Comment