Nguli wa muziki George Michael amefariki akiwa na umri wa miaka 53 DEC 25 2016. Alipata umaarufu wake miaka ya 80 na kuwa mmoja wa wanamuziki mashuhuri aliyefanikiwa pakubwa wakati wake
George Michael na Andrew Ridgeley waliunda bendi ya Wham! baada ya kujuana wakiwa shule. Walifanikiwa kutoa albamu mbili ambazo ziliorodheshwa bora zaidi huku nyimbo yao bora ikiwa ile ya Last Christmas, Club Tropicana na Wake Me Up Before You Go Go.
Michael alianza kuimba peke yake mwaka 1984 na nyimbo yake Careless Whisper, ambayo iligonga vyombo vya habari ilikuwa kibao chake alichojulikana nacho sana .Yeye na Ridgeley ni miongoni mwa walioimba katika tamasha la Live Aid mwaka 1985.Michael (kushoto) aliorodheshwa miongoni mwa waimbaji waliofuzu katika fainali ya tamasha la Live Aid katika uwanja wa Wembley pamoja na (kutoka kushoto hadi kulia) promota Harvey Goldsmith, Bono, Paul McCartney, Bob Geldof na Freddie Mercury.
Wakati wa uimbaji wake, Michael alifanikiwa pakubwa akishirikiana na nyota akiwemo Aretha Franklin (kulia),-wengine ni Elton John, Queen na Mary J Blige. Nyimbo yake alioimba na Franklin, I Knew You Were Waiting (For Me), ilipanda hadi nafasi ya kwanza katika maeneo yote ya Atlantic
Baada ya Wham!, kazi ya uimbaji ya George Michael ilianza kupata matuzo huku nyimbo zake zilizopanda katika chati ikiwemo Faith, Jesus To A Child na Fastlove.
Mashabiki wake maarufu walishirikisha Princess Diana wa Wales na wawili hao walikuwa marafiki . Baada ya kifo cha Diana 1997, Michael alihudhuria mazishi yake.
Kufuatia ufanisi wake miaka ya 1980s na mapema 1990s, maisha ya Michael na picha zake zilikumbwa na utata. Mwaka 1997, alikamatwa katika tukio la kushiriki ngono ndani ya choo mjini Los Angeles ambapo alikiri kuwa mpenzi wa jinsia moja.
Michael alikuwa na ukiwa wakati mpenzi wake wa muda mrefu Anselmo Feleppa alipofariki baada ya kutokwa na damu katika ubongo 1993. Miaka mitatu baadaye ,alikutana na Kenny Goss (katika picha ) na walikuwa pamoja hadi 2009.
George Michael and Ricky Gervais
Nyota huyo alikuwa akiugua katika miaka ya hivi karibuni ikiwemo homa ya mapafu ambayo ilimlazimu kulazwa katika hospitali ya Vienna 2011.Ziara ya mwisho ya muziki ya nyota Michael ilikuwa 2012, baada ya kuwatumbuiza mashabiki katika michezo ya Olimpiki ya 2012 mjini London katika sherehe ya kufunga michezo hiyo. Imeripotiwa kwamba kabla ya kifo chake nyota huyo alikuwa akitengeza albamu mpya ,miaka 12 baada ya kutoa kibao chake cha mwisho..........
"REST IN PEACE,THE LEGEND GEORGE MICHAEL"
No comments:
Post a Comment