YAHYA JAMMEH,KIONGOZI WA GAMBIA ALIYESHINDWA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2016,NCHINI HUMO..
Mamlaka nchini Gambia imekifunga kituo kimoja cha habari ambacho kimekuwa kikimkosoa rais wa taifa hilo Yahya Jammeh.
Maafisa wa Ujasusi waliagiza kituo cha habari cha Teranga FM kufungwa bila ya kutoa sababu ,alisema Emil Touray mkuu wa vyombo vya habari nchini humo.Hii ni ishara ya kwanza ya vita dhidi ya vyombo vya habari tangu bwana Jammeh kukataa kushindwa katika uchaguzi wa Disemba mosi mwaka 2016.
Bwana Jammeh alichukua mamlaka katika mapinduzi ya serikali mnamo mwaka 1994.
Awali alikuwa amekubali kushindwa na mfanyabiashara Adama Barrow(ambaye kiutaratibu ndiye mshindi halali), lakini akaenda mahakamani ili kupinga matokeo hayo,akisema uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu,licha ya hapo awali kushindwa na kumpongeza bwana barrow.
Tume ya uchaguzi nchini humo imesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki,hakukuwa na udanganyifu wa aina yeyote ile.
No comments:
Post a Comment