Thursday, November 3, 2016

MIMI NA HERMY B,NDIO ANGALAU TUNAISHI MAISHA MAZURI LICHA YA HILI GEMU KUWA LA HALI MBAYA KWA MAPRODUCERS WENGI WAKONGWE,MASTER J>>>>

JOACHIM KIMARIO(MASTER J)
MTAYARISHAJI(PRODUCER) MKONGWE WA MUZIKI NCHINI TANZANIA
Ni ukweli usiopingika kuwa, hakuna muziki pasipo kuwa na watayarishaji wa muziki – lakini wao ndio wamekuwa wakiongoza kuishi maisha ya chini Zaidi ukilinganisha na wasanii wa muziki.
Akiongea na kipindi cha Ladha 3600 ya EFM, mtayarishaji mkongwe wa muziki hapa nchini Master Jay amesema kuwa, kwa Bongo ni maproducer wachache wenye maisha ya kuendana na hadhi yao.
“Kati ya maproducer wanaoishi maisha mazuri hapa mjini ni mimi na Hermy B,” amesema Jay.
Master ameongeza kuwa, yeye alishtuka mapema ndio maana akaamua kuachana na kazi hiyo kutokana na kutoona faida halisi ya kazi hiyo wakati huo huo akiwa na familia inayomtegemea.
 
 

No comments:

Post a Comment