Lakini utafiti uliofanywa na wanasayansi unawapa wanaume ahuweni katika kuepuka lawama hizo, kwamba, kumbe siyo hiyari yao, bali ni maumbile.
Wanasayansi hao wamebaini kwamba, kwa sababu za kimaumbile ubongo wa wanaume unawalazimisha kulala muda mfupi baada ya kushiriki tendo la kujamiiana. Katika utafiti wao wanasayansi hao walibaini kwamba, kwa jinsi ubongo wa mwanaume ulivyotengenezwa, pale wanapomaliza tendo la kujamiiana na kufika kileleni kuna eneo linalozimika na kuwafanya kupata usingizi.
Wakati hilo likitokea kwa wanawake hali ni tofauti, kwani wao hubaki wakikodolea macho dari wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali lukuki, wakijihisi kutowaridhisha wapenzi wao.
Utafiti huo ulifanyika kwa kuhusisha kipimo cha kumulika, maarufu kama scan, ambapo kilitumika kuwamulika wanaume katika ubongo wao pale wanapofanya tendo la kujamiiana na baada ya kumaliza kujamiiana na kufika kileleni na kubaini kwamba, eneo linalojulikana kama cerebral cortex, eneo linalohusika na ‘fikra’ huzimika baada ya mwanaume kufika kileleni.
wanasayansi hao waliendelea kusema kwamba, wanawake hushangazwa sana na jambo hilo na ndio sababu hubaki wakiwashangaa wapenzi wao wanapolala baada ya kumaliza tendo ilo hali ya kuwa wao wakitaka zaidi….
Kwa hiyo sasa kutokana na sababu hiyo ama hizo kuu za kitafiti,nadhani hakuna sababu ya wanawake kutulaumu tena wanaume baada ya kumaliza tendo na kulala, kwa sababu hivi sasa wameshajua sababu, watuwache tupumuwe……
prepared and edited by
No comments:
Post a Comment