Tuesday, November 1, 2016

BAADA YA UHAKIKI WA WATUMISHI HEWA,UHAKIKI WA VYETI BANDIA KWA WATUMISHI SERIKALINI,SASA NI ZAMU YA UHAKIKI WA NDOA HEWA,SERIKALI HII SIO YA KUCHEZEA>>>>


STORY BY JULIET MACHA-JOURNALIST MACHA BLOG:-
Hewa imetawala kila sehemu kwenye nchi hii ndio maana serikali imeanza uhakiki wa vyeti vya ndoa kwa watumishi wa umma.
Hatua hiyo iliyowashtua watumishi wengi wa umma, imeelezwa kuwa ni mwendelezo wa harakati za serikali ya Rais John pombe Magufuli ,kuhakiki watumishi wa umma ili kuondokana na watumishi hewa na mambo hewa kwenye kila nyanja.
Wakati serikali ikianza na uhakiki wa vyeti vya ndoa, kazi ya uhakiki wa watumishi hewa na vyeti vyao vya elimu inaendelea sehemu mbalimbali nchini.
Kwa mujibu wa Gazeti la Tanzania Daima, serikali imeanzisha uhakiki huo nchi nzima kwa madai kuwa ,baadhi ya watumishi wa umma wamekuwa wakitoa taarifa za uongo kwamba wana ndoa ili kupata nauli na stahiki zingine za likizo wakati hawana ndoa.
Habari zaidi zinasema kuwa walimu wakuu wa shule zote za Wilaya ya Ilala wamepewa siku mbili kutekeleza agizo hilo kwa walimu wao.
Mmoja wa walimu hao ambaye ameomba jina lake lihifadhiwe, alilithibitishia gazeti hilo kuwa ametoa siku mbili kwa walimu wa shule yake wenye vyeti vya ndoa waviwasilishe kwake.
“Kweli tumepewa agizo hilo leo manispaa ya Ilala na tumetakiwa kuwasilisha vyeti hivyo kesho na tayari baadhi ya walimu wangu wamefanya hivyo leo na kesho zoezi hilo linakamilika,”
Alipoulizwa sababu ya kuwepo kwa zoezi hilo, mwalimu huyo alisema hajui lakini anahisi lina lengo la kudhibiti taarifa za uongo za watumishi wakati wa kuomba likizo.`
Wakati walimu wa shule za Ilala wakitakiwa kuwasilisha vyeti vyao vya ndoa, wilaya nyingine za Temeke, Kinondoni, Ubungo na Kigamboni hawana taarifa hizo.

No comments:

Post a Comment