Friday, October 28, 2016

NIMESTAAFU JAMANI NAOMBA NIACHWE NIPUMZIKE_JAKAYA MRISHO KIKWETE,RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA NNE NCHINI TANZANIA>>>>>

MHESHIMIWA DKT.JAKAYA MRISHO KIKWETE
RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA NNE NCHINI TANZANIA
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea masikitiko yake juu ya matumizi mabaya ya picha zake mitandaoni.
Kikwete ambaye alikuwa Rais wa awamu ya nne, kupitia ukurasa wake wa twitter amesema watu wamekuwa wakitumia picha hizo katika mambo yao ya kisiasa.
“Nasikitishwa sana na matumizi mabaya ya picha zangu mtandaoni hususan watu kunilisha maneno kwa kutaka kutimiza malengo yao ya kisiasa,” aliandika twitter.
Aliongeza, “Nimestaafu naomba niachwe nipumzike. Nisingependa kuhusishwa na siasa za mtandaoni dhidi ya Serikali. Namuunga mkono Rais na Serikali yake,”.
 

No comments:

Post a Comment