Monday, October 10, 2016

MAHAKAMA YAKUBALI MAOMBI YA WADHAMINI CUF,KUSIKILIZA SHAURI LAO DHIDI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI TANZANIA JAJI FRANCIS MUTUNGI>>>>>

MHESHIMIWA JUMA NASSORO,WAKILI WA WANA CUF,AKIONGEA NA WANAHABARI MBALIMBALI
 
STORY BY JULIE KAVISHE-JOURNALIST MACHA BLOG
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imetaja na kukubali maombi ya Bodi ya Baraza la Wadhamini la CUF dhidi ya Jaji Francis Mutungi ambapo yatasikilizwa wakati wowote wiki hii.
Katika maombi hayo namba 75 ya mwaka 2016 walalamikiwa wengine ni Prof. Ibrahim Lipumba na wanachama 12 wa chama hicho waliosimamishwa.
Bodi hiyo ya wadhamini ilifungua maombi hayo wiki iliyopita wakili wao akiwa ni Juma Nassoro wakiiomba mahakama itengue na kupitia uamuzi wa barua ya Jaji Mutungi kumtambua Lipumba kuwa mwenyekiti.
Akizungumza na wanahabari mara baada ya kutoka katika chumba cha kusikiliza shauri hilo, wakili Juma Nassoro amesema kuwa mahakama imekubali maombi hayo yaliyofunguliwa ya kuomba mahakama ifute barua ya msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, inayomtambua Lipumba kuwa mwenyekiti CUF.
Amesema pia mahakama imekubaliana na zuio lao la msajili kufanya kazi zake nje ya utaratibu ambao amepewa chini ya Sheria ya Vyama vya Siasa.
Baadhi ya wanachama wa Cuf wakiwa nje ya Mahakama Kuu.
MHESHIMIWA JAJI FRANCIS MUTUNGI,MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI TANZANIA
PROFFESOR IBRAHIM HARUNA LIPUMBA,MLALAMIKIWA/MLAUMIWA
 
BY MACHAS OFFICIAL SITE

No comments:

Post a Comment