MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA,WAZIRI MKUU WA ZAMANI TANZANIA,MJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA.
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametoa waraka akisema kitendo cha askari wa Jeshi la Polisi kuwakamata wakati wakiwa kwenye kikao cha ndani cha Chadema jana kimemuimarisha na kumpa nguvu zaidi ya kudai demokrasia.
Katika waraka wake kwa vyombo vya habari leo, Lowassa amesema anafurahishwa na kutiwa moyo na jinsi Watanzania walivyoipokea operesheni yao ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta) iliyopangwa kuanza kesho kutwa kwa maandamano na mikutano, lakini vitendo vya polisi vinawapa wasiwasi wananchi.
Lowassa, akiwa na Freeman Mbowe, ambaye ni mwenyekiti wa Chadema, John Mnyika (naibu katibu mkuu-Bara) na viongozi wengine wa chama hicho kikuu cha upinzani TANZANIA walikamatwa jana wakiwa kwenye kikao cha ndani kilichofanyika Hoteli ya Girrafe na baadae kwenda kituo kikuu cha polisi kwa mahojiano kabla ya kuachiwa na kutakiwa kwenda kituoni hapo kesho.
#MACHAS OFFICIAL SITE
No comments:
Post a Comment