Wednesday, August 31, 2016

CHADEMA WAMESITISHA MAANDAMANO YA AMANI(DEMONSTRATION) NA MIKUTANO YA HADHARA AMBAYO ILITAKIWA IFANYIKE KESHO SEPTEMBER 1 2016 NCHI NZIMA>>>>>

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kusitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike nchi nzima kesho Septemba Mosi yaliyopewa jina la UKUTA.
Akitangaza uamuzi huo, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amesema kuwa, wamefanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, BAKWATA, Baraza la Maaskofu, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Taasisi ya Mwalimu Nyerere,Jukwaa la Katiba na Jukwaa la wahariri na kuona kwamba wana kila sababu ya kusikiliza ushauri huo.
Aidha, maandamano hayo yameahirishwa kwa mwezi mmoja ili kwa viongozi wa dini watafute muafaka wa hali ya kisiasa nchini....
mheshimiwa FREEMAN HAIKAELI MBOWE,MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA..

No comments:

Post a Comment