Friday, July 1, 2016

Wema Sepetu Afungukia Ugomvi Wake na Aunt Ezekiel

STAA WA FILAMU TANZANIA "WEMA ISACK SEPETU" MADAMEEE
 
 
WEMA SEPETU & MRS MOSE IYOBO "AUNT EZEKIEL
 
 
STAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu amefungukia ugomvi ambao hutokea mara kwa mara na shosti wake ambaye pia ni muigizaji, Aunt Ezekiel usiingiliwe na mtu kwani wanapogombana tofauti zao wanazimaliza wenyewe na si mtu mwingine yeyote.

Akizungumzia swala hilo, Wema alisema kuwa, yeye na Aunt ni watu walio na  ukaribu mkubwa sana na wanaopendana hivyo inapotokea wanagombana huwa ni kitu kidogo kwao kwani huyamaliza na maisha yanaendelea kama kawaida.

“Jamani nyinyi mtuache tu, tunatibuana na Aunt, tunajuana vizuri sana ugomvi wetu ni wa mara kwa mara lakini tunamalizana wenyewe kwa sababu ukweli ni kwamba hatuwezi kukaa mbalimbali kwa muda mrefu kutokana na kupendana,” alisema Wema.
source: MOS
 
 
#MACHAS OFFICIAL SITE

No comments:

Post a Comment