Tuesday, November 29, 2016

SIASA TANZANIA: BAADA YA OPERESHENI UKUTA,CHADEMA KUJA NA HII,LENGO NI KUKIIMARISHA CHAMA ZAIDI>>>>

MHESHIMIWA FREEMAN HAIKAEL MBOWE
MWENYEKITI CHADEMA TAIFA...
Baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kuanzisha umoja wa kupinga udikteta Tanzania (UKUTA), Chadema imekuja na oparesheni nyingine inayokwenda kwa jina linaloitwa ‘Kata Funua’
Jina hilo limetangazwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa wilayani Masasi Mkoani Mtwara katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kanda kwenye wilaya hiyo huku akidai lengo la oparesheni hiyo ni kukipa chama hicho mafanikio katika uchaguzi wa serikali za mitaa hapo baadaye.
Kwa upande wake, Mjumbe wa kamati kuu Chadema, mheshimiwa Edward Lowassa aliwataka viongozi na wanachama wa chama hicho kuwa na umoja ili kufanikisha azma hiyo.
“Nawaomba ndugu zangu tuungane chini ya mwenyekiti wetu Freeman Mbowe na viongozi wengine tusimame imara tukiongoze chama chetu kwa umoja na mshikamano,” alisema lowassa.
 

No comments:

Post a Comment