Sunday, October 30, 2016

DONALD TRUMP,SIO MTU WA KUMCHEZEA KWENYE SWALA LA FEDHA,NI BILIONEA HATARI SANA,MAARUFU KAMA BILIONEA WA MAJENGO NCHINI MAREKANI,NA KWENYE NCHI MBALIMBALI DUNIANI>>>>>>

DONALD TRUMP,MGOMBEA URAIS MAREKANI KWA TIKETI YA REPUBLICAN
Ndege ya Donald Trump  Boeing 757, yenye thamani ya dola millioni 100.
Trump mara baada ya kushuka katika ndege yake binafsi(private jet)  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa San Jose.
Trump akiwa ofisini kwake katika jengo la  Trump Tower, Manhattan.
 Jengo la Trump Hotel ,Las Vegas
Trump Ocean Club International Hotel, ipo katika Jiji la Panama.
Trump International Beach Resort
Trump Ocean Club International Hotel.
Trump International Hotel & Tower Dubai
Trump Tower, Manhattan.
Donald Trump Tower amewekeza dola milioni 400, Dubai.
DONALD TRUMP JOHN alizaliwa mnamo 14 Juni 1946 huko Jamaica Estates, Queens akiwa ni mtoto wa pili kwenye familia ya watoto wanne wa familia ya Mary na Fred Trump na kukulia katika Jiji la New York, Marekani.....
-----
Upande wa baba yake (Fred Trump aliyefariki mwaka 1981), alikuwa mzaliwa wa Ujerumani na mama yake (Mary) ni mzaliwa wa Scottish.
Trump alianza kusoma katika Chuo Kikuu cha Fordham kilichopo Bronx mwaka 1964, miaka miwili baadaye alihamishiwa katika Shule ya mambo ya fedha na Uchumi ya Wharton iliyopo Chuo Kikuu cha Pennsylvania  ambako alihitimu shahada ya kwanza katika masuala ya uchumi mwaka 1968 kabla ya kujiunga na kufanya kazi kwenye kampuni ya familia yake iliyoitwa Elizabeth Trump & Son.
Mwaka 1971 Trump alikabidhiwa kuongoza makampuni na biashara za baba yake ambapo alipata mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi ambapo mpaka sasa ndiye mkurugenzi wake mkuu C.E.O.
Trump ambaye ni baba wa watoto watano, ni mfanyabiashara mkubwa na bilionea nchini Marekani, pia ni mtayarishaji wa vipindi vya televisheni.
Baadhi ya mali anazomiliki:-
Trump Ocean Club International Hotel and Tower lililopo Panama City, Panama
Trump Tower lililopo Manhattan
Wollman Rink lililoko Central Park
Trump Taj Mahal lililoko Atlantic City, New Jersey
Turnberry Hotel, iliyoko Ayrshire, Scotland
Trump Hotel Las Vegas
Trump International Hotel & Tower ya New York
Trump International Hotel & Tower ya Chicago
Trump International Hotel ya Las Vegas
Trump International Hotel ya Waikiki Beach Walk
 Trump SoHo ya New York
Trump International Hotel & Tower ya Toronto
Taasisi ya Donald J. Trump
Branding na licensing
Ndege kubwa ya Trump’s Boeing 757, maarufu kama “Trump Force One”.
Utajiri:-
Mwaka huu (2016), Jarida maarufu la Forbes lilikadiria utajiri wa mali za Trump kuwa unafikia dola bilioni 3.7. Ameweka rekodi ya kuwa mwanasiasa mwenye utajiri mkubwa zaidi kwenye historia ya nchi hiyo.
Ikijumulishwa na thamani ya kampuni yake (brand), Trump anakadiriwa kuwa na utajiri sasa wa dola bilioni 10 na kuwa tajiri namba 324 wa dunia na wa 156 kwa nchi ya Marekani.
Trump ni Mwenyekiti na Rais wa Shirika la Kibiashara la (Trump Organization) lenye makao yake makuu katikati ya Mji wa Manhattan ambalo linamiliki majengo mengi marefu, hoteli, kasino,  timu za gofu, ndege na miradi mbalimbali mikubwa ya maendeleo nchini Marekani na nje ya Marekani.
Ni mwanasiasa wa Chama cha Republican na anagombea urais wa Marekani kupitia chama hicho mwaka huu wa 2016, ambapo uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Novemba 8.
 
"kila la kheri wamarekani wote,katika kumpata kiongozi ataetokana na chaguo lenu"
 
prepared & edited by

No comments:

Post a Comment