Wednesday, July 13, 2016

Kituo Cha tabibu J.J Mwaka Chafutiwa Usajili, Wengine Wasimamishwa miezi 6 na kupewa onyo kali...

MWAKA J.J MKURUGENZI FOREPLAN HERBAL CLINIC AKIWA NA MSANII WA KIMATAIFA KUTOKA TANZANIA #DIAMOND PLATNUMZ
 
Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limekifutia usajili wake wa kutoa huduma za kitabibu, Kituo cha Tiba Asilia cha ForePlan Kliniki kilichopo Ilala Bungoni jijini Dar es salaam, kinachomilikiwa na Dkt. Juma Mwaka maarufu kama Dkt. Mwaka, kwa madai kuwa kimekiuka taratibu za kitabibu za tiba mbadala.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dkt. Edmund Kayombo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ukumbi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Akizungumza jijini Dar es salaam jana tarehe 12 july 2016 katika Mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk. Edmund Kayombo amesema kuwa kufutiwa kibali cha Dk. Mwaka kunatokana na sababu nyingi ambazo amekuwa akizikiuka licha ya kupewa maonyo na barua juu ya utoaji huduma zake.

Amesema sababu nyingine ni kuwa katika matangazo yake amesema anatoa tiba za kisasa wakati hiyo elimu hana ya kufanya hivyo.

Wengine waliofutiwa usajili ni Fadhaget Sanitarium kinachoendeshwa na Tabibu Fadhili Kabujanja pamoja na Mandai Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Abdallah Mandai

Hata hivyo limetoa adhabu mbalimbali kwa kituo cha Aman Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Esbon Baroshigwa, na Tabibu Castory Ndulu wa Kituo cha Ndulu Herbal Clinic wamepewa barua ya onyo.

Aidha wengine wamesimashwa kwa miezi sita ambao ni Tabibu John Lupimo wa Lupimo Suntarium Herbal Clinic pamoja na Tabibu Simon Rusigwa wa Sigwa Herbal Clinic.
 
 
 
#MACHAS OFFICIAL SITE

No comments:

Post a Comment