Showing posts with label DIAMOND PLATNUMZ. Show all posts
Showing posts with label DIAMOND PLATNUMZ. Show all posts

Wednesday, April 26, 2017

BONGO PLUG:UJUMBE MREFU WA DIAMOND PLATNUMZ KWENDA KWA RAY C…..

DIAMOND PLATNUMZ-WCB CHIEF
Boss wa WASAFI Record Lebel and Distribution Diamond Platnumz ametoa ushauri na sifa zake kwa msanii wa bongo fleva mkongwe Ray C ambaye hivi karibuni ameonyesha nia ya kuteka tena bongo fleva kupitia rekodi yake ya #Unanimaliza.
Ujumbe huu unasema “ Salaam dada angu @rayctanzania , siku ya leo nilitamani nikwambie maneno haya: Spirit ama juhudi unayoionyesha sasa inatia faraja sana, naamini sio kwa wapenda muziki wa Tanzania tu bali hata kwa watu mbalimbali…. Nafarijika kuona wimbo wako wa #Unanimaliza watu mbalimbali wameupokea vizuri, na nisiwe mnafiki hata mie ni miongoni mwa watu wanaoupenda wimbo huu wako mpya…. Ombi langu kwako usikubali kurudi nyuma tena, ijapokuwa sanaa zetu zina changamoto nyingi ila amini ni mitihani tu ya Mwenyez Mungu, ila ukiwa mvumilivu na kumuomba Muumba, itapita….niwaombe pia Vyombo vya Habari vyetu pendwa tuzidi kumsapoti dada etu, kwani naami kwa sapoti yenu, sapoti ya wadau mbalimbali na kuongeza juhudi kwake kutamfanya awe mfano bora, na kuamsha vijana wengi sana mitaani kwetu ambao pengine walijikatia tamaa kwa mambo mbalimbali….InshaAllah Mwenyez Mungu akusmamaie katika kazi zako na Maisha ya kila siku @rayctanzania “
Ray C naye alijibu “Mdogo wangu umenigusa sana nimetoa chozi, nashukuru sana kwa maneno yako ya faraja, Mungu ni mwema sana kwa kila jambo,maneno yako yamenipa nguvu na matumaini,Nashukuru sana sana”

Monday, February 27, 2017

ENTERTAINMENT: KWA NINI DIAMOND PLATNUMZ,ALIONA NI VYEMA KUJIUNGA #YOUTUBE-VEVO,LICHA YA KUWA APO AWALI HAKUPENDEZEWA? HAYA NDIYO MAJIBU YAKE>>>>

DIAMOND PLATNUMZ,-INTERNATIONAL MUSICIAN FROM TANZANIA
Diamond Platnumz ameeleza sababu iliyomfanya hatimaye kufungua akaunti ya Vevo baada ya kuikataa kwa muda. Wimbo wake, Marry You aliomshirikisha Ne-Yo ni wa kwanza kuwekwa kwenye akaunti hiyo, na sasa ina views zaidi ya milioni 4.
Kupitia Instagram, staa huyo amedai kuwa alikubali kujiunga na Vevo baada ya kujiridhisha kuwa atakuwa akipata treatment ile ile wanayopata wasanii wa Marekani;
 
Ameandika:
Kuna siku niliulizwa kwanini we haupo Vevo… Nikawambia: “uwepo wa msanii @VEVO anatakiwa msanii alipwe zaidi ya alivyokuwa analipwa kwenye Youtube channel ya kawaida.. Vevo wenyewe pia wamtambue kuwa kuna msanii anaitwa Nasibu Abdul aka Diamond toka Tandale, na pia anacholipwa msanii wa Marekani kwa view moja ama tangazo lolote liekwalo mwanzo ama lipitalo katikati pindi ya utazamaji wa video hyo basi nae anapaswa kulipwa hivyohivyo…na mbali tu ya kumlipa VEVO yapaswa kwa namna moja au nyingine kusaidia kupromote maana ni biashara yao wote na kila msanii ana shabiki zake na ukubwa na nafasi yake atokapo”…..hivyo nikawambia: “siku mkiniona nipo vevo basi jua nimeyakamilisha haya, vinginevyo wacha niendee kuokota senti mbili tatu, kwenye chanel yangu ya Youtube kawaida….
SABABU YA KUYASEMA HAYA: Ni kutaka kuwafahamisha ama kuwaamsha baadhi ya wasanii wenzangu watambue kuwa Mziki wetu hata kama hauko mkubwa saaaana ulimwenguni, ila Mwenyez Mungu kausaidia kuufikisha sehem flani, hivo wasanii lazma tujitambue na Tuwe na Misimamo na kazi zetu, vilevike umakini kwenye maamuzi ama hatua yoyote tutayoichkua juu ya sanaa zetu kwa sasa, maana tuliamualo leo linaweza kutujenga ama kutubomoa baadae… nafaham wasanii wengi hawakuwa wakilifaham hilo na badala yake kuingia @VEVO kupitia watu kati ama madalali na kuambulia status mtaani kuwa wako @VEVO ilhali nyuma kuna watu wanawadhurumu mamilioni ya pesa zitokanazo na jasho lao…” kwa uchungu wa kufaham namna gani inauma msanii ukinyonywa kazi yako ndio umenifanya nilizungumze hili leo, ila ukiona kwa namna moja au nyingine nimekosea Tafadhali mnisameh… -SIMBA #MALENGO

 

Wednesday, February 8, 2017

ENTERTAINMENT NEWS: SMART MUSICIAN FROM AFRICA, TANZANIA'S DIAMOND PLATNUMZ, JUST BEAT SHINING AND EXERCISING ITS SIZE, THIS IS AFTER HIS SONG "MARRY YOU" HAPPEN IN BLOG OF 50 CENT >>>

Diamond Platnumz believes that ,its objectives are increasingly fulfilled. One is to ensure that, his name transcends from Africa by going to other continents especially Europe and the United States.Through his song Marry You featuring Ne-Yo, slowly begins to tread,popular  Blog owned by 50 Cent..  Thisis50 That becomes the first video for the song By that hitmaker to be placed on the popular entertainment blogs in the US. With it,diamond   has already begun to get an interviews with British radio stations, including PulseRadio.

Thursday, December 22, 2016

SALLAM a.k.a MENDEZ ,AELEZEA ZILIPOFIKIA COLLABO ZA DIAMOND PLATNUMZ , RICK ROSS NA RIHANNA>>>>>

Hivi karibuni wakati anahojiwa kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, Diamond alitease ujio wa ngoma ambazo amewashikirisha wanamuziki heavyweight wa Marekani, Rick Ross na Rihanna.
Jumatano hii kupitia kipindi cha Campus Vibes cha Times FM, meneja wake, Sallam alifafanua zaidi kuhusu hatua iliyofikiwa ya collabo hizo. Sallam alidai kuwa collabo na Rick Ross imeshakalimika, huku ile ya Rihanna ikiwa kwenye hatua za mwisho kwakuwa tayari CV na historia ya Diamond imeshatumwa kwa uongozi wake kuweza kufikiwa maamuzi ya mwisho.
Kuhusu nyimbo alizoshirikishwa Diamond, Sallam alisema mwakwani itatoka ngoma aliyoshirikishwa na Burna Boy na Cassper Nyovest huku pia Dj Van wa Morocco akimshirikisha pamoja na msanii mkubwa wa Dubai.
Alidai kuwa kutokana na ubusy alionao hitmaker huyo wa Salome, imekuwa ngumu kupata muda wa kushoot video ya wimbo alioshirikishwa na msanii wa Jamaica, Alaine, wimbo alioshirikishwa na msanii wa Ivory Coast Serge Beynaud pamoja na kukamilisha wimbo anaoshirikishwa na rapper namba moja wa Cameroon, Stanley Enow.
Pia alidai kuwa Diamond atatumbuiza kwenye tuzo za CAF 2016, Alhamis ya January 5, 2017 mjini Abuja, Nigeria na pia kwenye ufunguzi wa kombe la mataifa ya Africa (Total Africa Cup of Nations),itakayofanyika nchini Gabon kuanzia January 14.

Thursday, December 8, 2016

DIAMOND PLATNUMZ,AZIDI KUVUNJA REKODI,KUWANIA TUZO ZA "AAMMA 2016" NCHINI AUSTRALIA>>>

Muziki wa Bongo Fleva unazidi kutoboa kwenye bara la Ulaya. Wimbo wa ‘Kidogo’ wa Diamond aliowashirikisha P Square umefanikiwa kutajwa kuwania tuzo za ‘AAMMA 2016’ za nchini Australia.
Diamond anawania tuzo hiyo kwenye kipengele cha ‘Song Of The Year 2016’ huku akiwania tuzo hiyo na msanii mwengine kutoka Afrika Mashariki, Bebe Cool na wasanii wengine kama Jidenna, Tekno, Tinnie Tempah, Davido, Drake na wengine.
Tuzo hizo hutolewa kwa wasanii wa Afrika au kwa nyimbo za wasanii wengine waliowashirikisha wasanii kutoka Afrika.
Hawa ni wasanii na nyimbo zao zinazowania tuzo hiyo....................
Ahmed Soultan – ANA O RASSI
Alicia Keys (Black Coffee) – IN COMMON (Black Coffee Remix)
B Wise (Dopmamine) – NO QUESTIONS
Bebe Cool – DEDE
Boddhi Satva + Teedra Moses (Boddhi Satva) – SKIN DIVER
Burna Boy (LeriQ) – PRE ME
Charlie Bucket + Blitz the Ambassador + Raashan Ahmad (Charlie Bucket) – ONE LIFE
Chip + Burna Boy (Jfem) – REACHING
Davido + Tinashe (Spellz) – HOW LONG
Diamond Platnumz + P-Square – KIDOGO DJ Maphorisa + DJ Buckz + Wizkid (DJ Maphorisa // DJ Buckz) – SOWETO BABY
Drake + Wizkid + Kyla (Nineteen85 + DJ Maphorisa) – ONE DANCE
Eugy + Mr Eazi (Team Salut) – DANCE FOR ME
Fuse ODG + Badshah + Zack Knight (Killbeatz) – BOMBAE
Fuse ODG + Shatta Wale (Killbeatz) – LAUGH OUT LOUD
Jay Rox + Thugga (Zone Fam) – GLORY
Jidenna (Jidenna) – LITTLE BIT MORE
Joey B (Kuvie) – U X ME
Legendury Beatz + Ceeza (Legendury Beatz) – LOVE AT FIRST SIGHT
Lola Rae (P2J) – ONE TIME
Major Lazer + Nyla + Fuse ODG (Major Lazer) – LIGHT IT UP
Maleek Berry (Maleek Berry) – KONTROL
Mi Casa + Yemi Alade (Maleek Berry) – GET THROUGH THIS
Moelogo + Sarkodie + Davido (P2J) – PENKELE REMIX
Muthoni the Drummer Queen + Kagwe Mungai (Kagwe Mungai) – HOT THIS YEAR
Okenyo (Badcop)- 10 FEET TALL
Patoranking + Sarkodie (Gospelondebeatz) – NO KISSING BABY
Remi + Sampa the Great (Sensible J) – FOR GOOD
Roberto + Reekado Banks + General Ozzy – DREAMS
Silvastone + Gory (Silvastone) – REAL MAN
Tekno (Krizbeatz) – PANA
Timaya (Kitwana Israel) – BANG BANG
Tinie Tempah + Wizkid (Bless Beats) – MAMACITA
Tiwa Savage + Busy Signal (Spellz) – KEY TO THE CITY REMIX
Tiwa Savage + Olamide (Don Jazzy) – STANDING OVATION
Tiwa Savage + Wizkid (P2J) – B.A.D.
Walshy Fire + Runtown + Wizkid + Machel Montano (Del B & Kickraux) – BEND DOWN PAUSE REMIX
Wizkid (Legendury Beatz) – FINAL (Baba Nla).............................


Monday, November 28, 2016

DIAMOND PLATNUMZ AZIDI KUNG'ARA KAMA JINA LAKE,HII APA NYINGINE TENA>>>>>

DIAMOND PLATNUMZ,MWANAMUZIKI MKALI WA KIMATAIFA KUTOKA TANZANIA
Diamond Platnumz ameshinda tuzo ya African Entertainment Legend Awards (AELA), za nchini Nigeria kwenye kipengele cha Best Collaboration (Africa) kutokana na wimbo wake Kidogo aliowashirikisha, P-Square.Tuzo hizo zimetolewa Jumapili hii jijini Lagos, Nigeria.
 
ABOUT (AELA).........
African Entertainment Legend Awards (AELA) is designed to recognize and celebrate personalities and entertainers who standout distinctively and remained consistent overtime in their various fields of entertainment. AELA is also geared towards giving support to young emerging and creative talents in Africa and Diaspora.
African Entertainment Legend Awards (AELA) is produced and packaged by Flexy Entertainment with the support and collaboration of Africa’s finest brands and entertainment lovers. It is an annual celebration of the most distinguished African Acts, in Music, Film production, Movies, Comedy , On Air personalities ,Brands, Entertainment Personalities, Broadcasting, Comedy, Fashion, Media, Modeling and Magazines.
It is indeed about blitz, style, glitz, razzmatazz and celebrating legends and true excellence in creative arts across Africa and diaspora.
This is undoubtedly the first and the most prestigious legendary award bringing African Entertainers, Government personalities, Organisations and Brands under one roof to be celebrated for their enormous contributions to the development of entertainment in Africa.