Juliana Rios Cantu ni kijana anayetokea nchini Mexico, na ametengeneza sidiria ambayo itaweza kukujulisha uwepo wa dalili za ugonjwa wa saratani ya matiti.Juliana Rios Cantu na wenzake watatu wanaounda kampuni ya Higia Technologies, wametengeneza sidiria iitwayo Eva, na kufanikiwa kushinda kiasi cha dola 20,000 kwenye mashindano yaliofanyika kwa kushirikisha wanafunzi wenye mawazo ya biashara.
Kufuatia ushindi huo uliohusisha mataifa yote duniani, Rais wa nchi yake ya Mexico Enrique Peña Nieto , amempongeza kijana huyo kwa kushinda katika mashindano hayo yaliyohusisha wanafunzi waliopo shuleni.
Tayari sidiria hiyo imefanyiwa majaribio na itafanyiwa vipimo vingine vya kimatibabu kabla ya wataalam wa ugonjwa wa saratani kuipendekeza kuwa njia ya kugundua saratani.Ili uweze kutambua kuwa una dalili za ugonjwa wa saratani basi utalazimika kuivaa kwa dakika 60 hadi 90 kwa wiki ili kupata vipimo vya sawa...
No comments:
Post a Comment