Friday, February 10, 2017

GREAT NEWS FROM TANZANIA: FINALLY MR. FREEMAN MBOWE RESPONSE, HAVING ASSOCIATED WITH ILLEGAL TRADE, THE DRUGS >>>>>

MHESHIMIWA MBOWE,AKIADDRESS TUHUMA DHIDI YAKE,ZILIZOTOLEWA NA MAKONDA
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa hon. Freeman Mbowe amekanusha tuhuma za kuhusika na dawa za kulevya ikiwa ni siku chache baada ya kutajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ndugu Paul Makonda, katika orodha ya watu 65 wanaodaiwa kuhusika na dawa za kulevya.
Akizungumza na wanahabari leo Mjini Dodoma ,mheshimiwa Mbowe amesema kuwa, hajawahi kujihusisha kwa kufanya biashara wala kutumia madawa za kulevya wakati wote katika maisha yake.
Pia Mbowe amesema kuwa, vita hiyo imechelewa sana kuanza kwani ilipaswa kuanza miaka mingi iliyopia, kwa kuwa imekuwa ikididimiza maendeleo ya Taifa.
Mbowe amesema kuwa, CHADEMA inaunga mkono vita dhidi ya dawa za kulevya na iko tayari kuungana na yeyote atakayeiendesha bila kujali chochote, lakini haiko tayari kuunga mkono vita yenye hila na chuki ndani yake.
Mbowe pia amesema, atamshitaki Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda kwa kumchafua ,kwa kuwa anaamini kuwa yeye hana hatia, bila kusubiri kusafishwa na polisi.
>>>>pia amesema kuwa,wito dhidi yake wa kuitwa polisi,haukufwata utaratibu,hivyo hatoenda mpaka taratibu zifuatwe...
 

No comments:

Post a Comment