Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hawezi kuzungumzia suala la kughushi vyeti kwa sababu majibu yake yapo mitandaoni suala hilo lilipoanzia.
Makonda amesema hayo Ijumaa alipoulizwa swali na mwanahabari wa Bongo5 (Yasin Ngi’tu) kuhusu uhakika wa taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa alinunua vyeti na kutumia jina lisilo lake.
“Maswali ya mitandaoni yanaishia mitandaoni siko hapa kupoteza focus (mwelekeo).Ukiona maneno mengi yanaibuka kwenye madawa ya kulevya ndiyo ujue vita imefika penyewe,” alisema paul c makonda.
SOURCE AMA CHANZO CHA TAARIFA:BONGO5.COM
No comments:
Post a Comment