Wednesday, January 25, 2017

HABARI KUU:WASOMALI 90,NA WAKENYA WAWILI WATIMULIWA NCHINI MAREKANI,MATAIFA SABA KIZUIZINI KUINGIA AMERICA>>>>>

HON. DONALD J. TRUMP-RAIS WA MAREKANI
Raia takriban 90 wa Somalia na wawili wa Kenya wametimuliwa kutoka Marekani saa chache baada ya taarifa kuibuka kwamba Rais Donald Trump atakabiliana na watu wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.
Wote waliwasili katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, lakini baadaye raia wa Somalia wakaendelea na safari hadi uwanja wa ndege wa Aden Abdulle mjini Mogadishu.
Msemaji wa serikali ya Kenya Eric Kiraithe ameliambia shirika la utangazaji uingereza BBC kwamba ni kweli raia hao wamefukuzwa Marekani, ingawa hakusema iwapo hatua hiyo imetokana na msimamo wa Bw Trump..
"Ni watu 90 kulingana na habari ambazo tulipewa. alisema, Wakati unaondolewa nchi fulani kurejeshwa kwenu, huwa unarejeshwa hadi kwenu direct,"
Kuhusu sababu iliyowafanya kufurushwa, Bw Kiraithe amesema: "Inategemea sheria za nchi ambayo walikuwa wamehamia (Marekani),"pia rais trump
Anatarajiwa kuweka masharti makali kwa raia wa mataifa saba ya Mashariki ya Kati na Afrika yenye idadi kubwa ya Waislamu wanaotafuta viza za kwenda Marekani.
Taarifa zinasema nchi hizo ni Syria, Iraq, Iran, Libya, Somalia, Sudan na Yemen.
Wakati wa kampeni yake ya urais, Donald Trump aliahidi kufanyia mageuzi suala la uhamiaji Marekani.
Aligusia pia ujenzi wa ukuta kati ya Mexico na Marekani kuzuia wahamiaji haramu na kuwapiga marufuku Waislamu kuingia katika taifa hilo kama sehemu ya vita dhidi ya ugaidi. Baadae alibadili msimamo kidogo na kufafanua kwamba watakachofanyiwa Waislamu ni kufanyiwa ukaguzi mkali kabla ya kuruhusiwa kuingia Marekani.
Awali, Bw Trump aliandika kwenye Twitter kueleza kusikitishwa kwake na kiwango cha juu cha ghasia na mauaji katika jiji la Chicago.
Vyombo vya habari wiki hii viliripoti kwamba tayari watu 228 wamepigwa risasi na wengine zaidi ya 40 kuuawa mwaka huu.
Bw Trump ameandika kwamba iwapo watawala wa Chicago hawatatatua tatizo hilo la mauaji, basi atawatuma 'Feds' akimaanisha maafisa wa FBI.

No comments:

Post a Comment