KUTOKA JIJINI Mbeya,nchini TANZANIA.
Bwana harusi, Samuel Mwakalobo aliyetoweka muda mfupi kabla ya kufunga ndoa na Given Mgaya katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Isanga jijini hapa, amerudi nyumbani kwao juzi.
Kaka wa bwana harusi huyo, Braison Mwakalobo ambaye ndiye aliyemlea, alisema alirudi nyumbani akiwa salama, lakini amepumzishwa bila kuulizwa lolote.
“Sijaongea naye lolote, yupo kwenye mapumziko, hivyo tunaomba mtuache kwanza,’’ Mwandemele alisema juzi. Mwakalobo (26) alizua taharuki Ijumaa ya Desemba 16, baada ya kutoonekana kanisani kufunga ndoa mbele ya Mchungaji Andagile Mwakijungu.
Kuhusu tukio hilo, Mchungaji Mwakijungu alisema ni la aina yake na linahitaji maombezi wala siyo kuzungumzazungumza hovyo. Alisema aliitangaza ndoa hiyo siku 21 kanisani hapo kwa mujibu wa sheria na hapakuwa na pingamizi lolote na kwamba Alhamisi jioni (siku moja kabla ya harusi) alikutana na wanandoa watarajiwa wote wawili na kuzungumza nao huku kila mmoja akiwa ni mwenye furaha na wakipeana miadi ya kuwahi ili wamalize mapema shughuli ya kuwaunganisha kimwili.
Mchungaji huyo alisema baada ya kuona tukio hilo limechukua sura mpya, alimuuliza bibi harusi kama kuna shida yoyote iliyojitokeza na kujibiwa kwamba hapakuwa na jambo lolote na kwamba hata yeye alishangaa kutomuona bwana wake wakati ndiye aliyempa hata fedha ya kwenda saluni.
given alisema, hee! kiukweli nimeshangazwa sana sijui hata nisemeje,ila namuachia mungu kwa maana bwana angu huyu,alinipa hela ya saluni na tulipeana ahadi za kupendana kwa dhati
No comments:
Post a Comment