Friday, October 21, 2016

WAZIRI WA ELIMU NCHINI TANZANIA MHE.PROFESA JOYCE NDALICHAKO,AIAGIZA BODI YA MIKOPO IREJESHE MFUMO AMA UTARATIBU WA ZAMANI WA UTOAJI MIKOPO KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU>>>>

MHESHIMIWA PROFESA.JOYCE NDALICHAKO
WAZIRI WA ELIMU NCHINI TANZANIA
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ameiagiza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kurejesha mfumo wa zamani wakutoa fedha kwa wanafunzi wa chuo.
Akizungumza katika mahojiano maalum Alhamisi hii katika runinga ya TBC Taifa, Waziri Ndalichako alikiri kutokea mapungufu katika mchakato wa ugawaji wa mikopo.
“Kama waziri nimeshaiagiza Bodi ya Mikopo kwamba kwa sababu wanafunzi tayari wapo mashuleni, warudi katika utaratibu ule wa zamani., kwa maana kwamba wanaangalia uhitaji ili mtu ambaye anastahili kupata apatiwe fedha bila kufanya makosa kwenye chakula angalau kwa muhula wa kwanza. Halafu kama kutakuwa kuna haja yakufanya kulingana na uwezo, vile vigezo viwekwe wazi na wanafunzi waelimishwe lakini lengo letu lipo pale pale kwamba wanafunzi wenye uhitaji watapatiwa mkopo,”
Waziri huyo alisema Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu wa Juu imelazimika kubadili mfumo wa utoaji mikopo ili kukabiliana na mapungufu mbalimbali ambayo yamekuwa yakijitokeza.
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na sintofahamu kubwa kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika vyuo vikuu nchini baada ya wengi wao kukosa mikopo huku wachache wakipewa kiasi kidogo ambacho kinadaiwa hakitoshelezi.
 
 

No comments:

Post a Comment