Thursday, October 13, 2016

WAANDAAJI WA DUME CHALLENGE, T-MARC WAZUNGUMZIA SAKATA LA SCORPION ‘MTOBOA MACHO>>>>>

SALIM NJWETE(SCORPION),MSHINDI WA DUME CHALLENGE COMPETITION 2012
Taasisi ya T-Marc Tanzania iliyoanzisha shindano la Dume Challenge, imetoa taarifa yake kufuatia mshindi wake katika msimu wa kwanza, Salim Njwete kuhusika kwenye tukio la kupora na kumtoboa macho, Said Ally Mrisho jijini Dar es Salaam.
Imesema imepokea taarifa hiyo kwa aibu kubwa.
Taasisi hiyo imekiri kuwa Njwete aliyeshinda shindano hilo alipewa kazi ya ubalozi wa kondomu za Dume kuanzia mwaka 2012 hadi 2014. “Njwete hata hivyo hajawahi kuwa na uhusiano na chapa hiyo tangu mwaka 2014,” imesema taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji, Diana Monika Kisaka. AIDHA TAASISI HIYO>>>>
“T-MARC inapenda pia kuthibitisha kuwa Salim Njwete alikuwa balozi wa mradi wa ‘Hakuna Wasichoweza Girls Empowerment Program’ mwaka 2014, ambao ulishamalizika. T-MARC haina tena uhusiano wowote, rasmi au vyovyote na Salim Njwete,” imeongeza taarifa hiyo.
“T-MARC inaamini kuwa haki itatendeka katika jambo ambalo Salim Njwete anashtakiwa.”
 
 

No comments:

Post a Comment